Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kwa nini Yesu alikubali hoi hoi hizo

    Kabla ya hapo Yesu alikuwa hajaruhusu hoi hoi kama hizo. Aliona mbele matokeo yake. Mambo hayo yangalisababisha kifo chake. Lakini alitamani kudhihirisha kujitoa kwake kafara ambako kungekuwa kilele cha utume wake kwa dunia iliyoanguka. Yeye aliye asili ya mfano wa Kondoo kwa tendo la hiari akajiweka, wakfu kama dhabihu. Kanisa lake katika vizazi vyote, lazima lihesabu kifo chake kuwa jambo muhimu la kutafakari na kujifunza kwa ndani. Kila jambo lihusulo kifo hicho lazima lithibitishe pasipo mashaka kabisa. Matukio yaliyotangulia kafara yake kuu lazima yaelekeze kwa kafara yenyewe. Baada ya thubuti kama ile ya maingilio yake Yerusalemu, macho ya watu wote yatafuata safari yake hadi kufikia mwisho wake. Maingilio hayo ya shangwe yatakuwa mazungumzo ya kila mtu na kumweka Yesu mawazoni mwa kila mtu. Baada ya kusulibishwa kwake, watu wengi watakumbuka mambo haya, na hivyo kuongozwa kuuchunguza unabii. Wengi watakirishwa kuwa hakika Yesu alikuwa ndiye Masihi.TVV 320.3

    Siku hii, iliyoonekana kwa wanafunzi kama siku ya ajabu katika maisha yao, ingetiwa giza la mawingu kama wangejua ilikuwa utangulizi wa kifo cha Bwana wao. Alikuwa amewaambia mara kwa mara kuhusu kafara yake, lakini katika ile furaha kuingia Yerusalemu walisahau maneno yake ya huzuni.TVV 320.4

    Isipokuwa tofauti chache tu, wale wote waliojiunga na msafara ule walishikwa na uvuvio wa saa ile. Shangwe ziliendelea kupazwa: “Hosana kwa Mwana wa Daudi. Abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana. Hosana aliye juu mbinguni.”TVV 321.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents