Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Udhalimu wa kifedha kazini mwa Mungu

    Makelele ya mnada, milio ya ng’ombe na kondoo, makelele ya njiwa pamoja na milio ya fedha, jinsi zilivyokuwa zikibadilishwa, vilikuwa ghasia kubwa. Ilikuwa fujo, kwamba maneno yaliyokuwa yakisemwa kwa Mwenyezi Mungu yalizimwa katika makelele hayo. Wayahudi walifurahia hekalu lao, nao waliyahesabu maneno yaliyosemwa kwa mzaha hekaluni kuwa ni makufuru. Lakini upendo wa fedha umewapumbaza. Wametangatanga, wakaacha utakatifu wa ibada iliyoanzishwa na Mungu mwenyewe. Popote Mungu anapoabudiwa huwa ni mahali patakatifu. Soma Kutoka 19:12, 13. Mzunguko wa hekalu la Mungu ungehesabiwa kuwa ni mahali patakatifu, penye kuheshimiwa. Lakini katika kushindania mapato ya udhalimu, yote hayo hayakujaliwa. Makuhani na wakuu wengine, wangekuwa wamenyamazisha makelele yaliyokuwa hekaluni; na kuwapa watu kielelezo cha uchaji wa kweli, badala ya kukaa na kutafuta mapato yao, wangewasaidia wale wanaotafuta sadaka. Lakini choyo kimewafanya kuwa wagumu wasiojali.TVV 81.1

    Katika sikukuu hii, walikuja watu, ambao walikuwa na upungufu wa vitu, na wenye dhiki vipofu, na vilema na viziwi walikuja. Wengine walikuwa wamechukuliwa katika vitanda, kama machela. Wengine wao hawakuweza kupata hata sadaka ndogo sana ya kuleta kwa Bwana. Hata hawakuweza kujinunulia chakula. Watu kama hawa walikatishwa tamaa kwa usemi wa makuhani. Makuhani walijivunia fahari yao, lakini hawakuwa na fadhili yoyote, wala huruma. Maskini, na wagonjwa, na wenye shida, hawakuonyeshwa huruma hata kidogo.TVV 81.2

    Yesu alipoingia hekaluni, aliona biashara haramu humo. Aliona taabu ya maskini ambao walikuwa wakifikiri kuwa, pasipo kumwaga damu, hakuna ondoleo la dhambi. Aliona uwanja wa hekalu, ambao ni mtakatifu, ukifanyiwa biashara haramu. Jambo fulani lapaswa kufanywa. Wenye kuabudu wanatoa sadaka zao bila kuelewa, kuwa wanawakilisha sadaka halisi itakayotolewa kwa kutosheleza. Kati yao alisimama yule ambaye anawakilishwa na sadaka hizi, lakini bila kutambulikana, wala kuheshimika. Aliona kuwa sadaka zinatolewa kwa njia ya kupotoshwa. Makuhani na wakuu hawakuwa na uhusiano wowote kati yao na Mungu. Kazi ya Kristo italeta tofauti kamili katika ibada.TVV 81.3

    Katika kuangalia, Kristo aliangalia mambo ya nyakati na vizazi na karne, aliona jinsi Makuhani na wakuu walivyokataza Injili isihubiriwe kwa maskini, na jinsi upendo wa Mungu ungalizuiwa usiwafikie watu, na namna watu wangalifanyia neema yake biashara. Kwa mambo kama haya, alibadilika sura, akaonekana kuwa mwenye chuki na hasira. Watu wakamwangalia. Macho ya wale waliokuwa wakifanya biashara haramu yakakazwa juu yake. Wakaona kuwa mtu huyu amesoma mawazo yao, na kugundua siri za mioyo yao. Wengine walijaribu kuficha nyuso zao.TVV 81.4

    Makelele ya wafanya biashara yalinyamaza. Ukimya ukawa mzito sana. Ikaonekana kama watu wamesimama mbele ya mahakarna ya Mungu. Wakimtazama Kristo waliona Uungu ukifunuliwa katika ubinadamu. Mtukufu wa mbinguni akasimama mbele yao kama Hakimu, jinsi atakavyosimama siku ya mwisho, bila kufunikwa na utukufu utakavyomfunika siku hiyo, lakini akiwa na uwezo ule ule wa kusoma siri za mioyo. Macho yake yakamkazia kila mtu. Sura yake ikaonekana kuwa juu ya wote, aking’aa kwa mng’ao wa Uungu, kama mwenye amri. Sauti yake wazi kama ilivyokuwa katika mlima wa Sinai, alipotangaza sheria, sauti hiyo ilisikika hekaluni, ikisema: “Ondoeni hapa mmeifanya nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.”TVV 82.1

    Yesu akiinua mjeledi wa kamba kwa hao waliokusanyika hapo, akaamuru wafanya biashara watoke hekaluni. Kwa ushujaa, kutumia mkono, alizipindua pindua meza za wabadilisha fedha. Fedha zikamwagika sakafuni. Hakuna aliyethubutu kumwuliza. Hakuna aliyeshughulika na habari za biashara tena. Yesu hakuwachapa na mjeledi wa kamba, lakini mjeledi uliokuwa mkononi mwake ulionekana kana kwamba ni upanga mkali unaometameta. Wakuu wa hekalu, makuhani, wabadili fedha, na wauza ng’ombe na kondoo, walikimbia pamoja na vitu vyao kutoka mahali hapo, wakiepuka kutoka mbele yake, kama wanaoepuka hukumu.TVV 82.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents