Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  31 — Mahubiri Mlimani

  Mara chache Kristo aliwafundisha wanafunzi wake peke yao. Kusudi lake lilikuwa kuwafundisha makutano ya watu wengi, maneno ya kuonya ya kusihi na ya kutia moyo, akitafuta kuwafaidia wale watakaokubaliana naye.TVV 161.1

  Mahubiri ya mlimani ijapokuwa yalitolewa kwa wanafunzi wake, yaliwafaa makutano. Baada ya kuwatia mikono wanafunzi, ambao ni mitume, Yesu alikwenda kando ya bahari. Asubuhi sana watu walianza kukusanyika. Waliposikia mambo makuu aliyotenda, walikuja kumsikiliza na kuponywa maradhi yao... uwezo ulikuwa ukimtoka wa kuwaponya wote. Marko 3:8; Luka 6:17-19.TVV 161.2

  Pwani nyembamba haikutosha watu wote hata kama wangalisimama, kwa hiyo Yesu aliketi chini kwenye majani, na watu wote pia waliketi chini kwenye majani.TVV 161.3

  Wanafunzi wake waliketi karibu naye wakitamani kusikiliza mafundisho yake, ambayo watawapelekea watu wa nchi zote ili kuwafundisha. Waliamini kuwa ufalme ulikuwa karibu kusimamishwa.TVV 161.4

  Makutano pia walijisikia hali hiyo hiyo. Watu walipokuwa wameketi majanini kando ya mlima, mawazo yao yalikuwa yakiwaza juu ya utukufu wa baadaye. Waandishi na Mafarisayo walikuwa wakitazamia wakati watakapojitawala na kuachana na Warumi ambao wanawachukia, na kufurahia fahari ya kujitawala katika enzi tukufu katika ulimwengu.TVV 161.5

  Wakulima na wavuvi masikini walitumaini kusikia kuwa watapata starehe mahali pengine kuliko wakati huu wanapoishi katika hali ya dhiki, katika vibanda vyao na kula chakula cha wasiwasi. Walitumaini kuwa Waisraeli watatukuzwa kuliko mataifa mengine ya dunia, maana wao ni taifa teule lililoteuliwa na Bwana, na Yerusalemu utainuliwa juu ya miji yote.TVV 161.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents