Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Pilato Asadiki kuna Njama

  Pilato hakuamini kuwa mshitakiwa alikula njama ya kupindua serikali. Ila aliamini kuwa kulikuwa na njama ya siri kumwangamiza mtu asiye na hatia. Akimgeukia Yesu alimwuliza; “Wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Mwokozi akamjibu: “Wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Mwokozi akamjibu: “Wewe wasema.” Aliposema hivyo uso wake uling’aa kana kwamba mwali wa jua umemulika juu yake.TVV 410.1

  Waliposikia jibu lake Kayafa alimwambia Pilato kuwa hata yeye ni shahidi kuwa Yesu amekubali kosa aliloshitakiwa nalo. Pilato akamwambia: “Husikii ni mambo mangapi wanayokushuhudia?” Lakini Yesu “Asimjibu hata neno moja.”TVV 410.2

  Akisimama nyuma ya Pilato, na kuonekana mbele ya wote, Kristo alisikia matusi yote; lakini kwa yale mashitaka yote ya uongo hakujibu neno. Alisimama imara bila kutikisiwa na mawimbi ya ghasia hiyo yote. Ilikuwa kana kwamba mawimbi mazito ya bahari yaliinuka, na kujibwaga kando yake lakini bila ya kumgusa. Kimya chake kulikuwa nuru iliyomulika kutoka mtu wa ndani mpaka mtu wa nje.TVV 410.3

  Pilato alishangaa. Mtu huyu hajitetei ili kujiokoa? Alipokuwa akimtazama Yesu, hakuamini kuwa alikuwa mbaya kiasi walichokuwa wanadai makuhani. Katika kukwepa fujo ya watu, Pilato alimchukua Yesu kando na kuhoji zaidi. “Je Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?”TVV 410.4

  Yesu hakujibu moja kwa moja. Roho Mtakatifu alikuwa akishindana na Pilato, kwa hiyo alimpa nafasi ili apate kukiri imani yake. Yesu aliuliza: “Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? Pilato alielewa maana ya maneno ya Kristo, lakini hakutaka kukiri ungamo lililokuwa linamsukuma moyoni. Akasema: Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?”TVV 410.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents