Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Injili Ilivyo Na Uwezo

  Kristo aliwapa wanafunzi wake ujumbe wake. Alisema Wafundishe watu “kuyashika yote niliyowaamuru ninyi;” Yale aliyosema siyo kwa mdomo tu, bali pia katika Agano la Kale yanahusika hapa. Hakuna nafasi kwa hadithi za mapokeo, mawazo ya watu, au sheria zilizopitishwa na mamlaka za kidini. “Torati na manabii,” pamoja na taarifa za maneno na matendo yake mwenyewe, ndiyo hazina inayopaswa kupewa ulimwengu.TVV 466.1

  Injili isitolewe kama kitu ambacho hakina uhai, bali itolewe kama kitu hai chenye kubadili maisha ya watu. Wale walioishi maisha ya yanayomchukiza Mungu hukubaliwa. Wakitubu atawajaza roho yake ya mbinguni, halafu huwatuma katika mahali pa watu wakorofi kutangaza rehema zake zisizo na kikomo. Kwa njia ya neema yake watu wanaweza kupokea tabia ya Kristo, na hufurahi katika pendo lake kuu.TVV 466.2

  Yesu hatosheki kutangaza mibaraka hii tu; bali huitoa kwa njia ile ipendezayo inayowavutia watu kuipata. Kwa hiyo watumishi wake watangaze kipawa hiki kisicho na kifani. Upendo wa Yesu wa ajabu utalainisha na kutiisha mioyo ya watu ambapo kuyakazia mafundisho hakutafanikisha lo lote. Maneno matupu hayawezi kuelezea. Kristo anahitaji kuchorwa katika kila mfuasi wake. Upendo uonekane wazi katika maisha ya kila mtu, upendo na uvumilivu wake, rehema zake na kweli vinapaswa kudhihirishwa katika ulimwengu.TVV 466.3

  Wanafunzi wa kwanza walijiandaa kwa kazi yao. Kabla ya siku ya Pentekoste walikusanyika pamoja na wakaondoa tofauti zao zote. Wakaomba kwa nia moja kwa imani na wakiwa na mzigo kwa roho za watu. Ndipo Roho Mtakatifu akamwagwa kwao, na watu maelfu waliongoka kwa siku moja.TVV 466.4

  Na ndivyo inavyoweza kuwa na sasa pia. Hebu Neno la Mungu na lihubiriwe. Hebu Wakristo na waondoe tofauti zao, wajitoe kwa Mungu, kuongoa watu waliopotea. Hebu kwa imani na waombe mibaraka nayo itakuja. Kumwagwa kwa roho katika siku za mitume ilikuwa “mvua ya vuli” na matokeo yalikuwa ya utukufu, lakini “mvua ya masika” itakuwa tele. (Yoeli 2:23.)TVV 466.5

  Wote wanaojiweka waklu nafsi mwili na Ii” I.».ikwaTVV 467.1

  Mungu daima watakuwa wanapokea uwezo mpya, wa kimwili na kiakili. Kwa kushirikiana na Kristo, katika udhaifu wa kibinadamu wanawezeshwa kutenda matendo ya Mwenyezi Mungu.TVV 467.2

  Mwokozi atamani kudhihirisha neema yake na kuwapa chapa ya tabia yake katika ulimwengu wote. Anatamani kuwafanya wanadamu wawe huru, safi na watakatifu. Kwa njia ya damu iliyomwagika kwa ajili ya ulimwengu, kuna ushindi wa kufikiwa ambao utamletea utukufu Mungu na Mwana Kondoo. Kristo “Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika.” Isaya 53:11.TVV 467.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents