Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    55 — Si Kujionyesha kwa Nje

    Tangu Yohana Mbatizaji alipohubiri, ilikuwa imepita miaka mitatu. Hubiri lake kuu lilikuwa: “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Mathayo 3:2. Wengi katika wale waliokataa ujumbe wa Yohana, na ambao walikuwa wakimpinga Yesu kwa kila hatua, walikuwa wakijipenyeza kidogo kidogo wakisema kuwa kazi yake imeanguka.TVV 285.1

    Yesu alijibu: “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuji-onyesha kwa nje, (kwa kuonyesha ishara) maana hawatasema: Tazama yuko hapa. Au yuko kulel Maana ufalme wa Mungu uko ndani yenu.” Ufalme wa Mungu huanza moyoni. Wala hautatangazwa kama ufalme wa dunia utangazwavyo.TVV 285.2

    “Siku zitakuja ambazo mtatamani kuona moja ya siku za Mwana wa Adamu, nanyi hamtaona.” Hamfahamu bahati mliyo nayo ya kuwa pamoja na mwenye asili ya uzima na nuru ya watu. Mtatazama nyuma na kuona bahati mliyokuwa nayo ya kuishi na kuongea pamoja na Mwana wa Mungu.TVV 285.3

    Wanafunzi hawakuelewa hayo mpaka baada ya kupaa kwake mbinguni na kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, ndipo wanafunzi walifahamu kwa ukamilifu juu ya kazi ya Mwokozi na tabia yake. Walifahamu kuwa walikuwa mbele ya Bwana wa utukufu. Tazama Yohana 1:14. Mawazo yao yalifunguliwa waelewe unabii pamoja na miujiza aliyofanya. Walifanana sawa na mtu anayeamka kutoka katika ndoto. Wanafunzi hawakuwa na wasiwasi kuhusu Maneno yake na kazi yake. Mafundisho yake yalifunguwa wazi katika mawazo kana kwamba ni mafunuo mapya. Biblia ikawa kana kwamba ni kitabu kipya kwao.TVV 285.4

    Basi kiasi wanafunzi walivyokuwa wakichunguza unabii unaomshuhudia Kristo, walivutwa wakawa katika umoja na Mungu na kujifunza kwake yeye aliyepanda mbinguni ili kukamilisha kazi aliyoianzisha hapa duniani. Wakasema unabii unaohusiana na tabia yake na kazi yake. Wakaona jinsi walivyoelewa unabii kidogo mno! Walipomwona akitembeatembea kati ya wanadamu, hawakuelewa jinsi alivyofanyika kuwa mwili. Hawakuweza kufahamu jinsi alivyokuwa, kwamba Uungu uwe ubinadamu. Lakini baada ya kuvuviwa na Roho Mtakatifu, walitamani namna gani kumwona tena, na jinsi gani walivyopenda afundishe ukweli ule kwao tena! Kristo alikuwa na maana gani aliposema: “Ninayo mengi ya kusema, kwenu, lakini hamwezi kiiyashika yote?” Yohana 16:12. Wakasikitika kwamba imani yao ilikuwa hafifu sana, hata hawakuweza kuelewa lolote.TVV 285.5

    Mwanadamu aliyesemwa na Yohana kuwa atakuja, alikaa nao muda wa miaka zaidi ya thelathini bila kuelewa kuwa ndiye aliyetumwa na Mungu. Wanafunzi waliruhusu hali ya kutokuamini iwazibe mioyo wasielewe kitu. Kila mara walisema: Kwa nini tuliruhusu mashaka na kukubali upinzani wa Marabi utuchafue mawazo, kiasi kwamba hatukutambua kuwa mkuu zaidi ya Musa Alikuwa kati yetu, ambaye ni mwenye hekima kuliko Sulemani, ndiye anayetufundisha? Masikio yetu yalikuwa mazito kiasi gani?TVV 286.1

    Wanafunzi wa Kristo walipofikishwa mabarazan., na kutupwa magerezani, walifurahi kwa kuhesabiwa kuwa wakosaji kwa ajili ya jina lake. Matendo 5:41.TVV 286.2

    Waliutambua utukufu wa Kristo, na wakachagua kumfuata na kuacha vitu vyote.TVV 286.3

    Ufalme wa Mungu hauwi kwa kujionyesha kwa mambo ya nje tu. Injili iliyo ya kweli haiwezi kufuatana na mfumo wa ulimwengu. Lakini leo makutano wanataka kumtawaza Bwana wetu awe mfalme wa duniani. Atawale katika mahakama ya ulimwengu, na katika mabunge, na kutawala masoko. Wataka awatawale akifuata kanuni za kibinadamu. Kwa kuwa sasa Kristo hayuko hapa kimwili, wataka wawe badala yake. Utawala wa jinsi hiyo ndiyo Wayahudi walitaka kuwa nao wakati wa Kristo. Lakini yeye alisema: “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu.” Yohana 18:36.TVV 286.4

    Utawala wa siku zile ambazo Kristo alikuwako, ni utawala ulioharibika na kuoza, wenye dhuluma, na wenye kuonea watu. Kila upande kulikuwa na malalamiko ya ufedhuli wa kila aina.TVV 286.5

    Walakini Kristo alijaribu kufanya matengenezo ya utawala huo, ambao ni wa haki, usio na uhasama. Yesu hakujiingiza na mambo ya kuwasahihisha wenye mamalaka wa siku hizo. Yeye aliyekuwa kielelezo chetu alijitenga na mambo ya sasa, na mambo ya serikali. Si kwamba alikuwa hajali mambo ya wanadamu, ila kwa sababu dawa yake haikutokana na mawazo ya wanadamu, wala kanuni za mambo ya nje nje. Dawa yake ni lazima iwe ile iponyayo mioyo ya watu kwanza.TVV 286.6

    Mambo ya kuponya mioyo ya watu hayategemei mahakama, wala mabaraza, wala mabunge. Utawala wa Yesu haujengwi juu ya mabunge, bali ni kuwa na hali ya ukristo na Kristo mwenyewe katika maisha ya mtu kwa kusaidiwa na Roho Mtakatifu. Hii ndiyo njia ya kuwa na uwezo wa kumwinua mwanadamu kutoka katika kudidimia kwake na kuwa hafifu kwake. Kumsaidia mtu katika kazi hii ni kusoma maandiko matakatifu, yaani neno la Mungu.TVV 287.1

    Sasa, kama ilivyokuwa siku za Kristo, kazi ya kujenga ufalme wa Mungu haitegemei msaada wa wakuu wa dunia hii, au sheria zilizotungwa na mabaraza ya duniani, bali hutegemea watu watawa wanaolitangaza neno la kweli la Mungu na kulifuata jinsi linavyosema, na kufuata mashauri ya Paulo: “Nimesulibiwa pamoja na Kristo, lakini ni hai; wala si mimi niliye hai, ila Kristo yu hai ndani yangu.” Wagalatia 2:20.TVV 287.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents