Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hofu ya Wanafunzi Ilitoweka!

    Wanafunzi hawakuwa na mashaka tena juu ya siku za usoni. Walifahamu kuwa Yesu yuko mbinguni, na ya kuwa fadhili zake ziko pamoja nao. Walijua kuwa walikuwa na rafiki karibu na kiti cha enzi cha Mungu, na walikuwa na hamu ya kuyapeleka maombi yao katika jina la Yesu. Kwa kicho waliomba walisujudu kuomba wakikariri ahadi yake, kwamba: “Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu . . . Ombeni, nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifu.” Yohana 16:23, 24. Na Pentekoste iliwaletea furaha timilifu mbele ya Mfariji, kama Kristo alivyoahidi.TVV 470.3

    Mbingu yote ilikuwa inangojea kumpokea Mwokozi. Alipopaa aliongoza njia, na umati wa mateka waliokombolewa wakati wa kufufuka kwake ukiwa unafuata. Na walipokaribia karibu na mji wa Mungu, changamoto ilitolewa na malaika wasindikizaji.TVV 470.4

    “Inueni vichwa vyenu, enyi malango;
    Inukeni, enyi malango ya milele;
    Mfalme wa utukufu apate kuingia.”
    TVV 470.5

    Kwa shangwe Mabawabu waliitikia:TVV 470.6

    Ni nani Mfalme wa utukufu?TVV 470.7

    Walisema hivi si kwa sababu hawamjui yeye Alikuwa ni nani bali walitamani kusikia jibu la kutukuza.TVV 470.8

    Bwana mwenye nguvu hodari,
    Bwana hodari wa vita!
    Inueni vichwa vyenu enyi malango.
    Naam, viinueni, enyi malango ya milele,
    Mfalme wa utukufu apate kuingia.
    TVV 470.9

    Kisha malango ya mji wa Mungu yalifunguliwa wazi, na jeshi la Malaika likaingia kwa shangwe za nyimbo. Majemadari wa majeshi ya malaika, na wana wa Mungu wanaowakilisha sayari za viumbe ambavyo havikuanguka dhambini ‘ walikusanyika ili kumkaribisha Mwokozi na kusherekea ushindi wake.TVV 471.1

    Lakini aliwapungia mkono akisema: Bado siyo sasa.” Aliingia mbele ya Mungu Baba. Akaonyesha makovu ya kichwa chake, ubavu uliochomwa, miguu iliyokuwa na majeraha; Akainua mikono yenye alama za misumari. Aliwaonyesha wale waliofufuka pamoja naye kama wawakilishi wa umati wa wale watakaofufuka kutoka makaburini akija mara ya pili. Kabla ya kuweka misingi ya dunia Baba na Mwana walishikana mikono wakaahidi kuwa Kristo atakuwa arbuni wa wanadamu. Pale msalabani Kristo alipolia “Imekwisha”, Alikuwa akimwambia Baba yake. Mapatano yalikuwa yamekamilishwa. Na sasa akatamka, Baba nimeikamilisha kazi ya ukombozi.TVV 471.2

    “Hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo.” Yohana 17:24.TVV 471.3

    Sauti ya Mungu ikatangaza kwamba haki imetimizwa na Shetani sasa ameshindwa. Wafuasi wa Kristo wanaotaabika na kujitahidi duniani wamekubalika “Katika huyo Mpendwa.” Waefeso 1:6. Mikono ya Baba ikamkumbatia Mwanaye, na tamko likatolewa: Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu.” Waebrania 1:6.TVV 471.4

    Mbingu ilionekana kujazwa kwa furaha, na sifa. Upendo ulikuwa umeshinda. Mpotevu amepatikana. Sauti zikajaa tele mbinguni zikitangaza kwa sauti nzuri zikisema: “Baraka, na heshima, na utukufu na uweza na nguvu una Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana Kondoo, hata milele na milele.” Ufunuo 5:13.TVV 471.5

    Kutoka katika hilo tukio la furaha ya mbinguni, mwangwi wa maneno ya Kristo huturudia duniani ukisema, “Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.” Yohana 20:17. Jamaa ya mbinguni imeunganika na jamaa ya duniani. Kwa ajili yetu Bwana wetu alipaa, na kwa ajili yetu anaishi. “Kwa sababu hii aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa njia ya yeye, maana yu hai siku zote ili awaombee.” Waebrania 7:25.TVV 471.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents