Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    84 — Kristo Aliyefufuka Atokea

    Wale wanafunzi wawili walipofika Yerusalemu waliingia kupitia katika lango la mashariki wakatembea kupitia barabara nyembamba wakimulikiwa na mng’ao wa mwezi, wakaenda hadi katika chumba cha juu mahali Yesu alipokula pasaka ya mwisho kabla ya kifo chake. Walijua kuwa ndugu zao wangekuwa hapo. Mlango ulikuwa umefungwa kabisa. Walibisha, lakini bila kusikia sauti. Palikuwa kimya. Hivyo walijitaja kwao, mlango ukafunguliwa kwa pole pole sana, wakaingia ndani, na mwingine asiyeonekana akaingia pamoja nao. Kisha mlango ukafungwa ili wapelelezi wasiingie.TVV 453.1

    Wasafiri hawa waliwakuta wale wengine walikuwa wote wameshikwa na msisimko. Sauti mle chumbani zilisema Bwana amefufuka kweli naye amemtokea Simoni! “Kisha wale wawili wakiwa wanahema kwa haraka haraka waliwaeleza jinsi Yesu alivyowatokea. Wengine walikuwa wakieleza kuwa haiwezekani kuwa kweli, wakati kwa ghafla Mtu mwingine akasimama mbele yao. Hakuna mgeni aliyekuwa amefunguliwa mlango, wala hakuna kishindo cha kutembea mtu kilichosikika akitembea huko nje. Wanafunzi wakashituka. Kisha, wakasikia sauti ya Bwana, kwa wazi na dhahiri “Amani iwe kwenu.”TVV 453.2

    Lakini wakashituka, na kuogopa sana wakidhani ya kwamba wameona roho. Ndipo “Akawaambia, Mbona mnafadhaika? na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa, ni mimi mwenyewe! Nishikeni shikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake.”TVV 453.3

    “Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?” Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Akakitwaa akala mbele yao. Ndipo wanafunzi walifurahi walipomwona Bwana. Imani ikachukua mahali pa kutoamini, na wakamkubali Mwokozi wao Aliyefufuka.TVV 453.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents