Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Imani katika Kristo ilimpatia hoja ya ajabu

  Mwokozi alitosheka na imani ya mwanamke huyu. Alikuwa ameijaribu imani yake. Aliona kuwa mtu aliyetengwa na kuhesabiwa kwamba ni mmizimu na Wayahudi, hakuwa jinsi hiyo, bali alikuwa mwana wa ufalme wa Mungu. Akiwa kama mtoto wa nyumbani, ilikuwa ni haki yake kushiriki mibaraka na zawadi zote za Mungu. Sasa Kristo alimpa haja yake akifunga fundisho lake kwa wanafunzi. akimgeukia mwanamke kwa uso wenye kung’aa na upendo mwingi, alisema: “Ee mwanamke, imani yako ni kuu, iwe kwako kama ulivyotaka.” Tangu saa ile binti yake akapona. Mwanamke aliondoka akimtukuza Mwokozi wake, na kufurahi kwa ajili ya kupatiwa haja yake.TVV 224.1

  Yesu alikwenda pande za Tiro na Sidoni kwa ajili ya kufanya mwujiza huu. Alipenda kumsaidia mwanamke huyu, na wakati huo huo kuwapa wanafunzi wake kielelezo cha fadhili zake wakati atakapoondoka. Alitaka kuwazoeza namna ya kuwahudumia watu wasiokuwa wa kabila lao.TVV 224.2

  Yesu alipenda kushindilia ukweli halisi, kwamba watu wa mataifa pia wana haki ya kuwa warithi pamoja na Wayahudi, na washiriki wenzao katika ahadi za Mungu katika Kristo kwa njia ya Injili. Waefeso 3:6. Katika kumponya mtumishi wa akida, na kuhubiri huko Sikar, Kristo alithibitisha kuwa hakuna kitu kinachowahusu Wayahudi peke yao, bila wengine, na sasa Yesu aliwaleta wanafunzi wake wakutane na wamizimu ambao walidhaniwa kuwa hawana haki kutendewa mema yale wanayotendewa Wayahudi. Aliwaonyesha kwamba upendo wake hauna upendeleo kwa kabila au kwa taifa fulani tu.TVV 224.3

  Wakati aliposema kuwa, “Sikutumwa, ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli, alisema kweli. Mwanamke huyu alikuwa mmoja wao wa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli, ambaye alistahili kuokolewa. Kristo alikuwa akifanya kazi ile ambayo wao waliipuzia.TVV 224.4

  Kitendo hiki kilifungua fahamu za wanafunzi zaidi sana, kuhusu kazi iliyowahusu kuwafanyia watu wa mataifa. Waliona watu ambao hawashughulikiwi, ambao wanamhitaji Mwokozi, na kutaka neno la kweli. Baadaye ukuta huu wa ubaguzi ulipovunjika wakati Kristo alipokufa, fundisho hili lilifahamika zaidi na zaidi, na wajumbe wa kristo walifanya kazi kubwa huko.TVV 224.5

  Kufika kwa Kristo huko Foeniki na mwujiza aliofanya huko ulifanya mvuto mkubwa, na ulikuwa na makusudi maalum. Leo, hali ile ile ya majivuno na chuki vimejenga kuta kubwa sana za ubaguzi kati ya Watu wa namna mbalimbali. watu wengi wametengwa mbali na injili. Lakini wao wasijione kuwa wametengwa mbali na Kristo.TVV 224.6

  Kwa imani mwanamke wa Kifoeniki alivunja ukuta huo na kujitupa miguuni mwa Kristo bila kujali utengano ulioko kati ya Wayahudi na mataifa. Bila kujali chochote alijitupa katika upendo wa Mwokozi. Kristo anatutaka tumtumaini hivyo. Baraka za wokovu na kwa kila mtu. Hakuna kitu kinachomzuia mtu asishiriki baraka hizi, isipokuwa mtu mwenyewe achague kuzikataa.TVV 225.1

  Ubaguzi ni chukizo kwa Mungu. Machoni pa Mungu watu wote wanalingana kabisa. “Naye alifanya kila taifa la wanadamu . . . akiisha kuwawekea nyakati alizoamuru . . . ” “Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, . . . kwa kuwa kila atakayeliitia Jina la bwana ataokoka.” Matendo 17:26, 27; Warumi 10:12, 13.TVV 225.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents