Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    26 — Siku za Shughuli na Raha katika Kapernaumu

    Katika vipindi vya mapumziko ya Yesu kwa safari zake, alikaa Kapernaumu katika pwani ya bahari ya Galilaya, pakajulikana kana kwamba ndio “kwao”. Mathayo 9:1. Pwani ya ziwa na vilima vilivyozunguka, kulikuwa na miji na vijiji vingi. Ziwani kulikuwa na mashua nyingi za wavuvi. Popote watu walikuwa na shughuli nyingi za maisha.TVV 135.1

    Mji wa kapernaumu ulikuwa kwenye njia kuu ya kutoka Dameski kwenda Yerusalemu, na Misri, pia kwenda upande wa bahari ya Mediterranean. Watu wengi walipitia katika mji wa Kapernaumu. Hapo Yesu aliweza kukutana na watu wa makabila na mataifa mbalimbali, na watu wa kila hali. Mafundisho yake yaliweza kuenezwa mahali mbalimbali na watu walioyasikia. Uchunguzi wa unabii uliwataharukisha wote waliohusika. Wakaanza kumfikiria Mwokozi. Malaika walikuwa wakitayarisha njia kwa ajili ya kazi yake. Mioyo yao iliguswa, na kumwelekea Mwokozi.TVV 135.2

    Katika Kapernaumu, yule mwana wa diwani ambaye aliponywa na Yesu, alikuwa shahidi wa uwezo wake. Mkuu wa mahakama na wenzake waliamini. Ilipojulikana kuwa Mwalimu alikuwako kati yao, mji mzima ulitaharuki. Siku ya Sabato mkutano mkubwa ulikusanyika, hata wakakosa nafasi.TVV 135.3

    Wote waliomsikia Mwokozi walishangaa kwa mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na uwezo mwingi. Aliwafundisha kama wenye mamlaka, wala si kama waandishi. Luka 4:32; Mathayo 7:29. Mafundisho ya waandishi na wazee yalikuwa ya baridi sana wala hayana nguvu. Walikuwa wakisema kuwa wanaieleza sheria, lakini hakuna mafunuo yoyote yaliyotoka kwa Mungu,, yenye kusisimua mioyo yao, na mioyo ya wasikilizaji wao.TVV 135.4

    Kazi ya Yesu ilikuwa kuifundisha kweli. Maneno yake yalimulika nuru katika mafundisho ya manabii, watu wakaona ukweli uliomo. Watu walikuwa hawajatambua maana ya maneno ya Mungu kama walivyotambua kwa mafundisho ya Yesu.TVV 136.1

    Yesu aliupamba ukweli wa neno la Mungu kwa njia ya kuulinganisha na hali halisi ya watu, kwa njia fupi. Watu wakaona wazi bila matatizo. Lugha yake ilikuwa safi, dhahiri, kama maji yatiririkayo. Sauti yake ilikuwa sawa na wimbo mtamu, ikilinganishwa na ya marabi.TVV 136.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents