Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kristo bado ni Mchutigaji wetu binafsi

  Msaidizi wetu ambaye hatuachi kamwe, hawezi kutuacha tupigane na majaribu sisi wenyewe, mpaka tushindwe. Ingawa sasa hatumwoni uso kwa uso, sikio la imani humsikia akisema: “Usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Nimejitwika huzuni zako, nimejitia katika mashindano yako nimejikinga katika majaribu yako. Ninajua machozi yako, na mimi pia nimelia. Masikitiko makuu kabisa ya wanadamu ninayafahamu. Wewe hukuachwa kamwe. Ingawa masikitiko yako hayasikiwi mahali popote duniani, nitazame mimi upate kuishi angalia.” Isaya 54:10.TVV 273.5

  Kwa kuwa sisi ni kipawa cha Baba yake, na zawadi ya kazi yake, Yesu hutupenda kama watoto wake. Anakupenda wewe. Mbingu haiwezi kutoa kitu kikubwa zaidi kuliko hiki kwa hiyo amini tu. Yesu aliwafikiri watu wote wa ulimwengu waliokoseshwa na wachungaji wanyonge. Yeye asema: “Ninao kondoo wasiokuwa wa zizi hili, inanipasa niwalete hao nao. Wataisikia sauti yangu kwa hiyo kutakuwa kundi moja na mchungaji mmoja.”TVV 273.6

  Kwa hiyo Baba anipenda, kwa kuwa nautoa uzima wangu, na nitautwaa tena .... Nina uwezo wa kuutoa, na nina uwezo wa kuutwaa tena. Yesu akiwa wa jamii ya wanadamu, alikuwa mtu wa mwili. Akiwa kama Mungu alikuwa ndiye asili ya uzima wa ulimwengu. Alishinda mauti. Lakini alitoa maisha yake, ih apate kuyatwaa tena. “Aliyejeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa makovu yetu .... kwa kupigwa kwake tumepona. Sisi sote kama kondoo waliopotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe na Bwana ameweka maovu yetu sisi sote.” Isaya 53-5, 6.TVV 274.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents