Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Yesu Kwa Kweli Hakuthaminiwa

    Wakati Yesu alipokuwa hayupo pamoja nao tena na wakajiona kama kondoo wasio na mchungaji, ndipo wakaanza kuona, jinsi ambavyo walikuwa waufuraishe moyo wake. Hawakumsukumia lawama tena Mariamu, bali wakajilaumu wao wenyewe. Loo, kama ingeliwezekana kufutilia mbali shutuma zao za awali, kuwaona maskini kuwa waliostahili zaidi lile tunzo kuliko Kristo! Walihuzunishwa mno na lile karipio walipokuwa wakiuondoa msalabani mwili wenye majeraha wa Bwana wao. Leo, ni watu wachache wanaofurahia yale yote Kristo aliyowafanyia. Kama wangefanya hivyo basi ule upendo mkuu wa Mariamu ungedhihirishwa. Hakuna ambacho kingefikiriwa kuwa cha thamani nmo kumpa Kristo, hakuna kujikana nafsi au kujitoa mhanga ambako kungeonekana kama kupita kiasi kwa ajili yake. Maneno yaliyosemwa kwa hasira, “Ni wa nini upotevu huu?” yalionyesha dhahiri kwa Kristo kafara kuu kuliko zote iliyowahi kutolewa karama yake Mwenyewe kuwa kipatanisho kwa ulimwengu uliopotea. Kwa mtazamo tu wa kibinadamu, mpango wa wokovu ni upotevu potovu waliseme zana. Hebu na jami ya mbinguni waiangalie kwa mshangao jamii ya wanadamu wanaokataa kutajirishwa kwa upendo usiyo na kifani uliodhihirishwa katika Kristo. Hebu kwa mshangao na waseme, kwa nini upotevu huu mkuu?TVV 315.3

    Lakini sadaka ya upatanisho kwa ulimwengu mpotevu ilikuwa iwe kamili, tele, na timilifu. Kafara ya Kristo ilikuwa tele na zaidi ili kuifikia kila roho. Siyo wote wanaookolewa; hata hivyo mpango wa ukombozi siyo upotevu kwa sababu tu haukufaulu kutimiliza yote yale yaliyokusudiwa kupatikana kwa ukarimu wake. Ni sharti wokovu uwepo tosha nakusaza.TVV 316.1

    Simon mwenye kuwakaribisha alishangaa kwa maneno ya Yesu, akasema kimoyomoyo, “Mtu huyu angelikuwa nabii angelijua kuwa mwanamke huyu anayemgusagusa ni wa aina gani; maana ni mwenye dhambi.”TVV 316.2

    Kwa sababu Kristo alimruhusu huyu mwanamke kumkaribia, na kwa vile tu hakumkatalia kwa hasira kuwa ni mwenye dhambi nyingi mno kiasi cha kutosameheka, na kwa sababu Kristo hakuonyesha kuwa alimtambua alivyoanguka. Simoni alishawishika kufikiri kuwa Kristo hakuwa nabii. Lakini ni kutokumjua Mungu na Kristo ndiko kulikomuongoza kufikiria kama alivyo waza.TVV 316.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents