Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hakuna mtoto wa Kifalme

  Katika Bethlehemu Yusufu na Mariamu hawakupata mlinzi yeyote wa kuwahudimia pamoja na mtoto wao, ambaye ni Mfalme. Hakuna heshima yoyote waliyopata. Yehova alikuwa katika kitanda kidogo embacho ni hori na wazazi wake ndio walikuwa walinzi wake peke yao. Je, hili ndilo angepaswa kutendewa, yule atakayewainua mataifa ya Yakobo, na kuwa nuru ya mataifa, mpaka mwisho? Isaya 49:6.TVV 30.5

  Walipofika katika nyumba, walimwona mtoto mchanga, akiwa na Mariamu mama yake. Walianguka wakamsujudia. Halafu walimtolea zawadi, ambazo ni dhahabu, na uvumba, na manemane. Lo, walikuwa na imani kubwa kiasi gani! Mamajusi bila kumwendea Herode kama alivyokusudia, walijiandaa kurudi kwao, baada ya kufaulu kumwona Masihi. Walikuwa wameonywa katika ndoto kuwa wasimrudie Herode. Wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.TVV 31.1

  Kwa njia ile ya ndoto Yusufu alionywa kwamba, amchukue mkewe Mariamu na mtoto Yesu wakiimbilie huko Misri. Yusufu akaondoka bila kukawia, akakimbilia mahali pa usalama.TVV 31.2

  Hoja ya mamajusi na hali ya kuchangamka iliyokuwapo, pamoja na wivu wa Herode viliwafanya watu watafakari kuhusu tukio hilo lilotukia, maana watu walichunguza unabii uhusikao.TVV 31.3

  Shetani alikazana kuzuia mwanga wa Mungu usiwaangazie walimwengu, huku akitumia hila yake ili iwezekane kumharibu mwokozi. Lakini Mungu asiyesinzia, wala kulala, aliandaa kimbilio katika nchi ya mataifa, ili Mariamu na mtoto wapate kukimbilia. Na kwa zawadi zilizotolewa na mamajusi, zilipatikana fcdha za kusafiria mpaka Misri” katika nchi ya ugeni.TVV 31.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents