Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  86 — “Enendeni . . . Mkawafanye Mataifa Yote”

  Kristo akiwa amesimama hatua chache kutoka kiti chake cha enzi cha mbinguni, alitoa agizo, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni, wafanye mataifa yote kuwa wanafunzi.” “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.” Marko 16:15. Maneno haya yalirudiwa mara kwa mara ili wanafunzi wapate kuona umuhimu wake. Nuru ya mbinguni lazima imulike kwa ukamilifu na nguvu kwa wakazi wote wa ulimwenguni.TVV 462.1

  Agizo hilo lilikuwa limetolewa kwa wale wanafunzi kumi na wawili kwanza katika chumba cha ghorofa, lakini sasa linatolewa kwa watu wengi zaidi. Katika mkutano huu uliofanyika katika mlima wa Galilaya waumini wote walioweza kuhudhuria walikuwepo. Malaika waliofika kaburini waliwakumbusha wanafunzi juu ya ahadi yake ya kukutana nao huko Galilaya. Ahadi hii pia ilirudiwa kwa waumini waliofika Yerusalemu wakati wa Pasaka na kwa kupitia kwao ahadi iliwafikia watu wote waliokuwa wanaomboleza kifo cha Bwana wao. Wote waliutazamia mkutano huu kwa hamu kubwa. Watu walikuja kutoka kila mahali wakiwa na mioyo yenye shauku.TVV 462.2

  Wakati ulipowadia kadiri ya waumini mia tano, walijikusanya vikundi vikundi kando ya mlima wakiwa na hamu ya kujua yote kutoka kwa wale waliomwona Kristo tangu kufufuka kwake.TVV 462.3

  Ghafla Yesu alisimama kati yao bila mtu kujua alitoka wapi na alifikaje. Wengi walikuwa hawajawahi kumwona, lakini mikono na miguu yake waliona alama za kusulibishwa; na walipomwona walimwabudu.TVV 462.4

  Lakini wengine walikuwa na mashaka. Na ndivyo itakavyokuwa siku zote. Kuna wale wanaona vigumu kuonyesha imani na hujiweka upande wa kutokuwa na imani. Nao hupoteza mengi kwa sababu ya kutoamini kwao.TVV 462.5

  Msingi wa sura hii hupatikana katika Mathayo 28:16-20 Huu ulikuwa mkutano pekee ambao Yesu alikuwa nao pamoja na wengi wa waumini baada ya kufufuka kwake. Maneno yake yaliyokuwa yanatoka katika kinywa kilichokuwa kimefungwa katika mauti, yaliwachangamsha. Sasa akatangaza kwamba “mamlaka yote” alikuwa amepewa. Mawazo ya wasikilizaji wake yaliinuliwa hadi dhana za juu zaidi za heshima na utukufu wake.TVV 462.6

  Maneno ya Kristo yalikuwa tangazo kwamba, dhabihu yake kwa ajili ya wenye dhambi, ilikuwa kamili na timilifu. Kazi aliyokuja kuifanya ulimwenguni imekamilika. Sasa alikuwa njiani kwenda kwa kiti cha enzi cha Mungu. Alikuwa ameanza kazi yake ya uombezi. Akiwa amevikwa utukufu kamili, Alitoa agizo, “Basi Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Mathayo 28:19, 20. Aliwaagiza wanafunzi wake wafundishe imani isiyokuwa na ubaguzi wa rangi wala nchi. Imani ihusuyo watu wote mataifa yote, na tabaka zote za watu.TVV 463.1

  Kristo alidhihirisha aina ya ufalme wake. Kusudi lake lilikuwa kuanzisha ufalme wa kiroho, na siyo mtawala wa kidunia katika kiti cha enzi cha Daudi. Aliwaambia waangalie yote aliyosema na kuyafunua kama Masihi na jinsi watu walivyomkataa, yalivyotumia. Aliyayasema kuhusu, kudhalalishwa, mateso na kifo chake yamethibitika. Siku ya tatu alifufuka tena. Katika mambo haya yote unabii ulikuwa umetimizwa.TVV 463.2

  Kristo aliwaagiza, wanafunzi wake wafanye kazi aliyowaachia kuanzia Yerusalemu. Yerusalemu palikuwa ndipo mahali pa unyenyekevu wake kwa ajili ya jamii ya wanadamu. Ni wachache waliokuwa wametambua jinsi mbingu ilivyoikaribia dunia wakati Yesu alipokuwa miongoni, mwao. Kazi ya wanafunzi lazima ianzie Yerusalemu. Wanafunzi wangeweza kuomba mahali pazuri zaidi pa kuanzia kazi, lakini hawakufanya ombi kama hilo. Kristo alikuwa ametawanya mbegu ya ukweli, nayo itatoa mavuno tele. Nafasi ya kwanza ya msamaha lazima itolewe kwa wauaji wa Mwokozi.TVV 463.3

  Wengi katika Yerusalemu walimwamini Yesu, kwa siri na wengi pia walipotoshwa na udanganyifu wa makuhani na wakuu. Watu kama hao walitakiwa watubishwe. Wakati Yerusalemu nzima ilikuwa inataharuki kwa sababu ya matukio ya majuma machache yaliyopita, mahubiri ya injili yangefanya mwamko mkubwa.TVV 463.4

  Lakini kazi isingekomea hapo. Kazi ingeendelea mpaka, kona zote. Kristo alikuwa amewaambia wanafunzi wake kuwa. Ingawa taifa la Israeli limenikataa kama Maandiko yalivyotabiri, bado watakuwa na nafasi nyingine ya kumkubali Mwana wa Mungu. Kwenu ninyi wanafunzi wangu nawakabidhi ujumbe wa, rehema. Lazima utolewe kwanza kwa Waisraeli, halafu kwa mataifa yote na lugha na jamaa. Waaminio wote lazima wakusanywe katika kanisa moja.TVV 464.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents