Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uwezo Mpya watawala

  Wakati roho inapojitoa kwa Kristo, uwezo mpya hutawala moyo wake. Badiliko hupatikana ambalo mtu hawezi kulileta. Mtu anapojitoa kwa Kristo, Kristo huwa ngome yake hasa, iliyomsaidia kati fujo za ulimwengu; akiazimu kwamba hakuna mamlaka yatakajulikana kwake ila yake mwenyewe, yaani hakuna mtawala, ila yeye tu. Hivyo mtu anapolindwa na mbingu namna hiyo, huwa asiyewezekana kushindwa na mashambulio ya Shetani. Lakini tusipojitolea kamili kutawaliwa na Kristo, tutashindwa na mwovu. Sio lazima kwamba tuchague njia za Shetani ndipo atutawale, ila tu tusipojali kuunganika kabisa na utawala wa nuru, na kushiriki kikamilifu na wajumbe wa mbinguni, Shetani atafanya makao yake katika mioyo yetu. Ulinzi peke yake kwa majeshi maovu ni kumfanya Kristo awe na makao ya kudumu katika mioyo yetu, kwa njia ya imani ya kutaka haki yake. Tusipoambatanisha uhai wetu kwa Mungu hatutaweza kuzuia hali ya ubinafsi na majaribu ya kutenda dhambi. Kwa muda kitambo tunaweza kuacha mazoea yetu mabaya, lakini bila kujitoa kwa Kristo dakika kwa dakika, na kuendelea kushirikiana na Kristo, tutakuwa katika hali ya kushindwa na Shetani, na mwisho tutatenda apendavyo yeye. Hali ya mwisho ya mtu huyo itakuwa mbaya kuliko kwanza.” Hivyo ndivyo itakuwa kwa kizazi hiki kiovu. Hakuna waliokuwa wakaidi zaidi ya wale waliokaidi mwito wa rehema. Onekano la kawaida la dhambi ya kumtukana Roho Mtakatifu ni kule kuzidi kukaidi mwito wa mbinguni wenye rehema wa kutubu.TVV 176.2

  Katika kumkataa Kristo, Wayahudi walitenda dhambi isiyosamehewa, na kwa kukataa mwito wa rehema, tunaweza kutenda dhambi ya namna ile ile. Tunamweka Bwana Yesu katika aibu mbele ya Shetani na mbele ya viumbe wote wa mbinguni; na katika malimwengu yote wakati tunapokataa ujumbe wake wa rehema badala yake hutega masikio yetu kusikiliza mambo yanayowavuta watu mbali na Kristo. Mtu yeyote afanyaye mambo kama hayo, hawezi kupata msamaha wa dhambi zake, na mwisho hupoteza nia yote ya kupatanishwa na Mungu.TVV 176.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents