Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Makuhani na wakuu wanyamazishwa

    Wakisimama katika hali ya kutahayari, makuhani, wakuu na waandishi walikosa jambo la kusema mbele ya Kristo. Watu wengine walisimama kando wakiwacheka watu hawa wenye kiburi na majivuno wakiwa wameshindwa.TVV 332.1

    Mambo yote ya Kristo yalikuwa ya maana tupu na mvuto wake ulikuwa, uendelee kukumbukwa kwa kiasi kikubwa hata baada ya kusulubiwa kwake, na kupaa mbinguni. Watu wengi waliamini na kumfuata kwa ajili ya mambo ya siku hiyo. Tofauti baina ya Yesu na Kuhani Mkuu ilionekana wazi kwa jinsi walivyokuwa wakizungumza. Mkuu wa hekalu alijivika kwa heshima na fahari sana. Kichwani alivaa taji lililong’ara, nywele na ndevu zikiwa na mvi kutokana na umri wake. Mbele ya huyu mwenye majivuno, alisimama Mtukufu wa mbinguni bila mapambo yo yote, uso wake umefadhaika, wenye kuonyesha uvumilivu, na uaminifu. Huku akionyesha heshima na huruma. Watu wengi walioyasikia maneno yake na kuona matendo yake siku ile hekaluni walimwamini moyoni mwao kuwa ni nabii wa Mungu. Lakini kadiri watu walivyomfuata, ndivyo chuki ya Makuhani ilivyozidi juu yake.TVV 332.2

    Halikuwa kusudi la Kristo kuwaaibisha adui zake jinsi hiyo. Alikuwa na fundisho muhimu la kuwafundisha. Kule kudai kutotambua ubatizo wa Yohana Mbatizaji, kulimpa nafasi ya kusema mengi zaidi kwao na kuwadhihirishia hali zao, na kuongeza onyo jingine. “Mnafikiri nini?” Mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Akamwambia mtoto wa kwanza: “Mtoto nenda leo shambani ukalime. Akajibu, nitakwenda, wala asiende. Akamwambia na mwingine: Mwanangu, nenda leo shambani ukalime, akakataa, lakini baadaye akajuta na kwenda. Ni yupi katika hao aliyefanya mapenzi ya babaye?”TVV 332.3

    Swala hili liliwatupa wasikilizaji wake kando ya ngome yao. Mara moja walijibu “Yule aliyekwenda kulima.” Yesu akawakazia macho akawajibu kwa ujasiri na kusema: “Amini nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu katika kuingia kwenye ufalme wa Mungu. Maana Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, wala hamkumwamini, ila watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi mlipoona hivyo hamkutubu, ili mmwamini baadaye.”TVV 332.4

    Makuhani na wakuu hawakuweza kumjibu Kristo isipokuwa kama ipasavyo; na hivyo alipata jibu kuwa mwana aliyekataa kulima, walakini baadaye akaenda. Na ambaye alikuwa mfano wa watoza ushuru na makahaba. Yohana alipokuja na kuhubiri toba, watoza ushuru walimwamini na kubatizwa.TVV 333.1

    Mwana wa pili asiyekwenda kulima ni mfano wa waongozi wa Wayahudi ambao hawakukiri kuwa Yohana alitumwa na Mungu. Walipinga “shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye.” Luka 7:30. Wayahudi walikuwa sawa na mwana aliyekataa kulima, wakijidai kukubali, lakini wakitenda kinyume cha maungamo yao.TVV 333.2

    Makuhani na wakuu waliendelea kuwa kimya. Lakini Kristo alisema: “Sikieni mfano mwingine: Mkulima mmoja alifanya bustani yake, akaizungushia ugo, akachimba shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akawakabidhi watunzaji wake, akasafiri katika nchi za mbali. Wakati wa matunda watunzaji wakawakamata watumishi wale, wakampiga mmoja, na kumwua mwingine, na kumpiga mawe mwingine. Tena akatuma watumishi wake zaidi ya wale wa kwanza, wakawatenda kama walivyowatenda wa kwaaza. Mwisho wa yote alimtuma mwanawe, akisema kuwa huyu watamjali. Lakini watunzaji walipomwona, waliambiana. Huyu ndiye mrithi wa yote, basi na tumwue na kutwaa urithi wake. Walimshika na kumtupa katika shinikizo na kumchinja. Je, Bwana wa shamba hili atawatendaje waangalizi wale?”TVV 333.3

    Makuhani na wazee wakajibu: “Atawaangamiza waovu hao, na kuwaweka watunzaji wengine, ambao watatoa matunda kwa wakati wake.” Wasemaji hao waliona kuwa sasa wametoa hukumu inayowahusu wao wenyewe. Jinsi ambavyo watunza shamba walivyopaswa kutoa matunda kwa wakati wake, vivyo hivyo na watu wa Mungu walipaswa kuishi maisha ya kweli kufuatana na hadhi takatifu waliyo nayo. Lakini kama wale watunza shamba walivyowaua watumishi wa Bwana, ndivyo Wayahudi walivyowaua manabii waliotumwa kwao na Mungu ili kuwatubisha.TVV 333.4

    Hivyo maana ya mfano wa wakulima wale, haukuweza kubishiwa. Mwana mpendwa ambaye alitumwa na Mungu mwishowe, kwa watumishi wakaidi wakamkamata na kumwua, makuhani waliona wazi yaliyokuwa yanamkabili Yesu. Katika adhabu iliyowafika watumishi wasiyo na shukurani Kulidhihirika yaliyokuwa yanawasubiri wale ambao wangemwua Kristo.TVV 333.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents