Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maisha ya Afya ni Sehemu ya Injili

    Katika namna ya Mwokozi kuponya kulikuwa na mafundisho kwa wanafunzi wake. Uponyaji ulitoka tu kwa Uwezo wa yule Mponyaji mkuu, lakini Kristo alitumia njia za kawaida tu za kuponya. Alifundisha kuwa ugonjwa huletwa na kuvunjwa kanuni za Mungu, sheria za kiroho na za kimwili. Matatizo ya watu ulimwenguni yangaliepukika kama watu wangeishi kulingana na mpango wa Muumbaji. Alifundisha kuwa afya njema ni zawadi ya utii kwa kanuni za Mungu. Mganga Mkuu alikuwa amezungumza na watu wake kutoka wingu la moto, “Kwamba utaisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake,... mimi sitatia juu yako maradhi yo yote” kwa kuwa mimi ndimi BWANA nikuponyaye.” (Kutoka 15:26.) Kwa wagonjwa tunaweza kuwapa dawa Mungu alizoziweka katika mimea, na kuwaelekeza kwake mwenye uzima na aliye Mponyaji hasa. Tuwafundishe kuamini katika Mponyaji Mkuu na kutegemea uwezo wake.TVV 465.2

    Ni pale tu tunaposhiriki katika upendo wa Kristo kwa imani ndipo nguvu ziletazo uzima zitakapotiririka kutoka kwetu kwenda kwa watu wengine. Kulikuwa na sehemu zingine pengine ambapo Mwokozi hakuweza kufanya miujiza yake kwa sababu ya kutoamini kwao. Vivyo hivyo sasa kutoamini kanisa hulitenga kutoka kwa Msaidizi wa mbinguni. Kwa kanisa kutokuwa na imani humsikitisha Mungu na kumnyang’anya utukufu wake Uhai wa kanisa hutegemea uaminifu wake katika kutekeleza utume wa Bwana. Mahali ambapo hakuna juhudi ya kuwahudumia wengine upendo hupoa na imani hufifia. Malaika hushangaa kwa sababu ya watu kukosa shukrani kwa upendo wa Mungu. Mama na baba wangejisikiaje kama mtoto wao aliyepotea katika baridi na theluji alitekelezwa aangamie na watu ambao wangalimsaidia? Mateso ya kila mtu ni mateso ya Mtoto wa Mungu, na wale wasiojali kuwasaidia wanadamu wenzao wanaoangamia husababisha hasira takatifu ya Mungu.TVV 465.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents