Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Nafasi ya Mwisho ya yuda Kutubu

    Katika yote yale Yesu aliyosema kwa wanafunzi wake, kulikuwa na kitu fulani ambacho Yuda moyoni hakukubaliana nacho. Chini ya mvuto wake, chachu ya chuki ilikuwa ikifanya kazi yake. Yesu aliona kuwa Shetani alikuwa amefungua njia ya kuwashawishi wanafunzi wengine. Walakini Yuda hakudhihirisha wazi manung’uniko yo yote yale mpaka siku ya karamu nyumbani kwa Simoni. Mariamu alipompaka Yesu mafuta, ndipo Yuda akadhihirisha tamaa yake. Kwa kemeo la Kristo kiburi kilichojeruhiwa na kutaka kulipiza kisasi vilibomoa ukuta wa kinga moyoni mwa Yuda. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa kila anayedumu katika kucheza na dhambi. Lakini Yuda alikuwa bado kufanywa mgumu. Hata baada ya kuahidi mara mbili kumsaliti Mwokozi, bado kulikuwa na nafasi ya toba. Wakati wa kula Pasaka Yesu alimjumuhisha Yuda katika huduma yake kwa wanafunzi wake. Lakini hata hivyo wito wa mwisho wa upendo haukujaliwa. Miguu iliyooshwa na Yesu iliondoka kwenda kufanya kazi ya usaliti.TVV 405.2

    Yuda alifikiri kuwa ikiwa Yesu atasulibishwa, basi lazima jambo hilo litekelezwe. Wala kitendo chake hicho hakitabadili kitu. Na kama Yesu hatakufa, basi itakuwa kumalazimisha ajitoe Mwenyewe. Yuda alihesabu kuwa alikuwa amechukua hataua dhati katika kumsaliti Bwana wake. Yuda hakudhani kuwa Yesu ataruhusu akamatwe. Katika kumsaliti Yesu, Yuda alikusudia kumfundisha Yesu somo. Alikusudia kumfanya Mwokozi aanze kumheshimu. Mara kwa mara Mafarisayo na waandishi waliposhika mawe kutaka kumpiga, alitoweka. Na kwa vile alifanikiwa kutoweka mara nyingi, bila shaka hataruhusu ashikwe.TVV 405.3

    Yuda alikusudia kujaribu mambo. Ikiwa kweli Yesu alikuwa Masihi, watu watamtawaza kuwa mfalme. Yuda angepata sifa ya kumweka mfalme katika kiti cha enzi cha Daudi, na jambo hili lingempatia nafasi ya kuwa kaaribu na Kristo katika ufalme ujao. Katika bustani, Yuda aliwambia watu wale waliokuja kumkamata Yesu kwamba “Mkamateni.” (Mathayo 26:48.) Aliamini kuwa Kristo ataponyoka. Na kama wangemlaumu angewaambia kuwa, Sikuwaambieni kwamba, mkamateni sana?TVV 406.1

    Kwa mshangao Yuda alimwona Mwokozi akiruhusu akamatwe. Katika kila hatua alitazamia kuwa yesu atawaonyesha uwezo wake, kwa kujifunua kama Mwana wa Mungu. Lakini saa zilipopita bila kuona chao chote, hofu kuu ilimpata msaliti kuona kuwa amemuuza Bwana wake auwawe. Kadiri hukumu ya Yesu ilivyokaribia Yuda hakuweza kuvumilia hatia ya dhamiri yake. Kwa ghafula sauti iliyokauka ikasikika katika ukumbi ule: Hana hatia; Kayafa, muachie! Umbo refu la Yuda lilionekana likipenya katika umati wa watu waliopigwa na butwaa. Uso wake ulionyesha mfadhaiko, na jasho lilimtoka usoni. Kwa kasi alikiendea kiti cha hukumu na kutupa mbele ya kuhani mkuu vipande vya fedha vilivyokuwa gharama ya kumsaliti Bwana wake. Akikamata joho la Kayafa, alimsihi amuachie Yesu. Kwa ghadhabu kayafa alimsukuma, lakini hakujua la kufanya. Uongo wa makuhani ulifunuliwa. Walikuwa wamemhonga huyu mwanafunzi kumsaliti Bwana wake.TVV 406.2

    Yuda alisema, “Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.” Lakini kuhani baada ya kutulia akasema “Basi, haya yanatupasa nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.” Mathayo 27:4. Makuhani waliona vema kumtumia Yuda kama chombo chao, lakini walidharau ubaya wake.TVV 406.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents