Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kujiinua na kuanguka kwa Petro

  Petro alitembea majini salama alipokuwa akimwangalia Yesu; lakini alipogeuza macho yake na kuwatazama wenzake katika mashua, macho yake yalitoka kwa Yesu ambaye ndiye Mwokozi wake. Mawimbi yaliinuka juu sana, naye aliogopa. Kwa kitambo kidogo Kristo alitoweka katika macho yake, na imani yake ikatatanika, akaanza kudidimia. Lakini mawimbi yalipozungumza na mauti, Petro aliinua macho yake katika maji yenye hasira, akalia na kusema, “Bwana, niokoe.” Yesu akanyosha mkono wake, akisema, “Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?”TVV 209.1

  Petro na Bwana wake walitembea wakishikana mikono wakaingia mashuani. Sasa Petro alitulia. Alikuwa karibu kupoteza maisha yake kwa ajili ya kutoamini kwake, na kwa ajili ya kujivuna.TVV 209.2

  Matatizo yanapotokea ni mara ngapi huangalia juu ya mawimbi badala ya kumwangalia mwokozi! Maji ya kiburi huingia katika roho zetu. Yesu hawezi kutuita tumfuate, kisha akatuacha. Asema, “msiogope.” ” . . Upitapo majini, mimi nitakuwa pamoja nawe; Upitapo katika mito, haitakugharikisha . . . Mimi ni Bwana Mungu wako, Mtakatifu wa Israeli, Mungu wako, na Mwokozi wako . . . ” Isaya 43:1-3.TVV 209.3

  Katika msukosuko huu wa maji Yesu alitaka kumfundisha Petro kwamba usalama wake ulitegemea uaminifu wake na mng’ang’anio wake juu ya Mungu. Katika majaribu yafananayo na dhoruba usalama wake ni kumtazama Mwokozi peke yake. Alipojidhani kuwa ana uwezo, Petro alikuwa dhaifu kabisa. Kama angelijifunza fundisho lile la baharini, asingalishindwa wakati jaribu kubwa lilipomjia.TVV 209.4

  Mungu huwafundisha watoto wake siku kwa siku. Katika matukio mbalimbali ya kila siku, huwatayarisha ili waweze kufanya sehemu yao katika mambo makuu anayowaandalia. Tunaweza kudhani kuwa tunasimama imara sasa, wala hatutatikisika. Tunaweza kusema kwa uthabiti kuwa hakuna kitakachobabaisha imani yangu kwa Mungu na kwa neno lake. Lakini Shetani anapanga kupata njia katika hali ya mazoea yetu ili kutushambulia na kutubabaisha. Tunapofahamu makasoro yetu, na kutazamisha kwa Mwokozi hali zetu ili atusaidie, ndipo tutatembea katika usalama.TVV 209.5

  Mara moja tu Yesu alipozungumza mashuani, dhoruba ilikoma, na mashua ikafika pwani salama, wakafika mahali walipokusudia. Wanafunzi wake na watu wengine waliokuwa mashuani, walimsujudia Yesu kwa shukrani kubwa, huku wakisema, “Kwa kweli wewe ni Mwana wa Mungu.”TVV 209.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents