Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shetani alikuwa akijaribu kumfikia Kristo

  Shetani alikuwa akijaribu kunikatisha Yesu tamaa na kumfanya aache kazi yake, na Petro alikuwa akitoa sauti ya jaribu. Mkuu wa maovu , aliyekuwa mwenye wazo hilo lililotamkwa na Petro, ndiye alikuwa mwenye kusudi hilo. Shetani alikuwa amemwambia Kristo kuwa atampa milki zote za dunia kwa sharti la kuacha njia yake ya kujinyima na kujidhili. Sasa alitaka Petro akaze macho yake juu ya utukufu wa ulimwengu, ili asiutazame msalaba. Alimjaribu Yesu kwa njia ya Petro.TVV 235.3

  Lakini Mwokozi hakulijali jambo hilo, mawazo yake yalikuwa juu ya wanafunzi wake. Shetani alijiingiza kati ya Petro na Bwana wake. Maneno ya Kristo yalisemwa kwa mtu anayejaribu kutenda mtu na Mwokozi wake. “Nenda nyuma yangu, Shetani.” Wacha nikabiliane na Petro, nipate kumdhihirishia upendo wangu.TVV 235.4

  Hilo lilikuwa fundisho chungu ambalo Petro alifundishwa, lakini pote pote. Njia ya Kristo ni ya maumivu na unyenyekevu. Lakini ni katika tanuru la moto, ndipo wanafunzi wataona mibaraka yake. Zamani alikuwa ameandika: “Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe” 1 Petro 4:13.TVV 236.1

  Sasa Yesu aliwaeleza wanafunzi wake kuwa maisha yake ya kujinyima,, na ya kimaskini, ni kielelezo cha maisha ambayo lazima waishi. Alisema: “Mtu yeyote atakaye kunifuata lazima ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake kila siku anifuate.” Msalaba ulikuwa ukitumika katika utawala wa Kirumi. Ulikuwa kitu cha uchungu sana, na kifo chake kilikuwa cha ukatili kuliko vyote. Wahalifu waliohusika kwa kifo cha msalaba, iliwapasa kujichukulia msalaba mpaka mahali pa kusulubiwa. Kila mara walipobebeshwa misalaba walifurukuta sana na kutaka kujiokoa. Maneno ya Kristo kwa wanafuzi wake ingawa waliyafahamu kigizagiza, yaliwaonyesha mauti ya Kristo.TVV 236.2

  Maneno ya Kristo hayakuonyesha zaidi ya hali ya kujitoa kuliko hayo. Lakini hayo yote yalimpasa kwa ajili yao. Aliacha maisha ya mbinguni , akaja kuishi katika hali hafifu na ya matatizo, na mwisho kufa kifo cha aibu. Aliyekuwa wa fahari zote za mbinguni akawa maskini, ili kwa umaskini wake, tupate kuwa matajiri. yatupasa kufuata hatua alizopitia.TVV 236.3

  Upendo wa aroho za watu, maana yake ni kuisulubisha nafsi. Mtu aliye mtoto wa Mungu, angejiona kuwa yeye ni kiungo katika mnyororo wa kuongoa roho zilizopotea. Mkristo amejitoa nafsi yake kwa Mungu, na katika tabia yake humdhihirisha Kristo ulimwenguni.TVV 236.4

  “Mtu atakayejitahidi kujiokoa mwenyewe atajipoteza, na atakayejitoa nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili atajiokoa” Ubinafsi ni mauti. Moyo ukishindwa kusukuma damu mpaka mikononi au kichwani, utapoteza nguvu zake upesi. Hivyo ndivyo ilivyo na upendo wa Kristo huenea katika mwili mzima. Sisi tu viungo kila mtu kwa mwenzake, na mtu anayekataa kushirikisha imani yake atapotea. “Itamfaidia nini mtu, kuupata ulimwengu wote, na kupoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?”TVV 236.5

  Kristo alionyesha kuja kwake katika utukufu kwa wanafunzi wake, akija na majeshi ya mbinguni, halafu Yesu alisema” Atakuja kumlipa kila mtu kadiri ya kazi yake ilivyo.” Kwa kuwatia moyo alisema:“Amini nawaambieni, kuna watu wasimamao hapa ambao hawataonja mauti mpaka watakapomwona Mwana wa Adamu akija kaatika ufalme wake.”TVV 236.6

  Lakini wanafunzi wake hawakuelewa maneno yake, mambo yao yalikuwa yakiuangalia umaskini wake, unyenyekevu wake, na mateso yake. Je, hawatamwona BWANA wao akitawazwa katika kiti cha enzi cha Daudi? Je, badala ya kutawazwa, inawezekana kwa Kristo kukataliwa na watu, na kuuawa? Huzuni iliwajaa mioyoni mwao; maana ilionekana kitu acha ajabu kuwa Mwana wa Mungu kupita katika matatizo ya namna hiyo. Kwa nini ajihatarishe kwenda Yerusalemu kukabiliana na mambo kama hayo? Kwa nini ajitolee kuingia katika hali hiyo, na kuwaacha wanafunzi wake gizani, wakihangaika katika mashaka kama vile walivyokuwa kabla ya kujua?TVV 237.1

  Katika mkoa wa Kaisaria Filipi wanafuzi waliongea kwamba, Kristo hana la kuongopa juu ya Wayahudi, au juu ya Warumi. Mbona asifanye kazi hapo tu? Mbona ajitolee mwenyewe kwenda kufa? Ilakuwaje kuwa atausimamisha ufalme ambao milango ya kuzimu haitaushinda? Jambo hili ni fumbo.TVV 237.2

  Sasa walikuwa safarini wakienda katika mji ule ambako wataona masikitiko makuu. Walikuwa wakizungumza polepole, kwa mioyo mizito kuhusu mambo yaliyo mbele yao. Labda jambo fulani litatokea la kuzuia mambo haya. Hivyo walikuwa na wasiwasi, wakiogopa mambo yatakayotokea katika siku sita za giza zijazo.TVV 237.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents