Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  10 — Sauti Nyikani

  Kutoka katika watu waaminifu wa Israeli, ndimo mtangulizi wa Yesu alimotokea. Mzee Zakaria aliyekuwa kuhani, na mkewe Elizabeti, wote wawili walikuwa watawa. Na katika maisha yao ya utulivu, nuru iliwaangazia, kama nyota zinazoangaza katika giza. Kwa wazee hawa wawili, walipewa ahadi ya kuzaa mtoto, wa kiume; ambaye atatangulia mbele ya Bwana, ili kumtengenezea njia.”TVV 46.1

  Zakaria alikuwa amekwenda Yerusalemu ili kuhudumu kwa juma lake moja katika hekalu. Akiwa amesimama madhabahuni katika patakatifu, ghafla alimwona malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu. Zakaria amekuwa akikuombea kuja kwa Mwokozi kwa muda mrefu. Sasa sala hizi karibu zitajibiwa.TVV 46.2

  Zakaria alipata habari ya kufurahisha: Kwamba, “Usiogope, Zakaria; maana sala zako zimesikiwa, mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yohana. . . . Atakuwa mkuu mbele za Bwana, naye hatakunywa mvinyo, au kileo cho chote, naye atajazwa na Roho Mtakatifu. . . . Naye, atatangulia mbele ya Bwana mwenye nguvu za Eliya, ili kuwageuza baba kuelekea watoto wao, na wakaidi kuelekea hekima ya watawa, kutayarisha watu kwa ajili ya kuja kwake Bwana. Zakaria akasema kwa malaika, Nitajuaje jambo hili? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ameendelea kuzeeka.?”TVV 46.3

  Kwa muda kitambo mzee huyu alisahau vile Mungu alivyoahidi, kwamba anao uwezo wa kutimiza kila jambo. Tofauti yake ya kutoamini na ile ya Mariamu ni kubwa kiasi gani! Mariamu alisema, “Tazama mimi ni mjakazi wako Bwana, iwe kama usemavyo.” Luka 1:38. Kuzaliwa kwa mwana wa Zakaria, kama vile kuzaliwa kwa mwana wa Ibrahimu, na kwa Mariamu kulikusudiwa kutoka fundisho kubwa. Kwamba: lile tusiloweza kulifanya sisi hufanywa kwa uwezo wa Mungu ndani ya kila mtu anayeamini. Kwa njia ya imani, mwana aliyeahidiwa alizaliwa. Kwa njia ya imani uwezo wa kiroho hupatikana. Na sisi huwezeshwa kufanya kazi ya haki.TVV 46.4

  Miaka mia tano iliyopita, malaika Gabriel alikuwa amemjulisha Daniel unabii unaoendelea mpaka kwa kuzaliwa kwa Kristo. Kule kujua kuwa wakati wa kuja kwa Kristo kumekaribia, ndiko kulimfanya Zakaria aombe kuhusu kutokea kwa Masihi kudhihirike Sasa malaika yule yule aliyetoa unabii huu amekuja ili akutangaze kutimia kwake.TVV 47.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents