Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Udhalimu wa Hukumu ya Kristo

  Baraza la Sanhedrin lilikuwa limemhukumia Yesu kufa, lakini ilikuwa kinyume cha Wayahudi, kumhukumu mshtakiwa wakati wa usiku. Kisheria hukumu ilitolewa tu wakati wa mchana na mbele ya Baraza lililohudhuriwa na wajumbe wake wote. Hata hivyo Mwokozi sasa alitendewa kama mhalifu aliyehukumiwa, na watu duni. Yesu alipitishwa huku na huko, katika uwanja wa jumba la kuhani mpaka chumba cha askari, na huku akidhihakiwa kutokana na madai ya kuwa Mwana wa Mungu. Maneno aliyosema kuwa watamwona “akija mawinguni kutoka mbinguni”, yalikaririwa mara nyingi kwa dhihaka. Alipokuwa amefungiwa chumbani akingojea kuhukumiwa, hakulindwa asitendewe vibaya na wahuni, na hivyo wahuni walimtendea kila aina ya ufedhuli walivyoweza. Hali ya Kristo ya utawa iliwachochea kwa hasira. Huruma na haki vilikanyagwa chini. Hakuna mfungwa aliyepata kutendewa kama alivyotendewa Mwana wa Mungu. Lakini pigo lililoumiza zaidi kuliko ambavyo mkono wa adui ungeleteleza. Wakati alipokuwa akihojiwa na Kayafa, Kristo alikuwa amekanwa na mmoja wa wanafunzi wake.TVV 398.5

  Petro na Yohana walikuwa wamethubutu kufuata kwa mbali kundi lililokuwa limemkamata Yesu. Makuhani walimtambua Yohana, na kumruhusu aingie katika ukumbi, wakitumaini kuwa akiona jinsi wanavyomtesa, atamkana na kusema kuwa yeye siye Mwana wa Mungu. Yohana alimtambulisha Petro, naye akaingia ndani pia. Pale nje ya ukumbi waliwasha moto, maana ilikuwa baridi, kabla ya mapumziko. Kikundi cha watu wakakusanyika hapo na Petro naye bila kujali akasogea na kuchanganyika nao na kuketi akidhani kuwa atachukuliwa kuwa ni mmoja wapo wa mkutano waliokuwa wamemleta Yesu kuhukumiwa.TVV 399.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents