Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maneno ya Kristo yafarakisha wengi

    Jaribio lilikuwa zito sana. Hoi hoi na makusudi ya watu waliofikiri kumtawaza yesu kwa nguvu awe mfalme wao vilizimika. Maongezi hayo yalifunua macho yao. Wakaona kuwa kwa kushikamana naye hawataambulia chochote cha dunia hii. Wamekubaliana na uwezo wake wa kutenda miujiza, lakini hawawezi kukubaliana maisha yake ya kujinyima. Kama hataweza kuwaondoa katika utawala wa Kirumi, hawatashughulika naye kwa vyovyote.TVV 216.3

    Yesu aliwaambia dhahiri; “Baadhi yenu hamwamini” Akaongeza kusema, “Kwa hiyo nawaambieni, hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba yangu” Wasipovutwa kumjia ni kwa sababu mioyo yao haikumkubali Roho Mtakatifu awaongoze.TVV 216.4

    Kwa maonyo ya wazi hivi, hata sasa mioyo ya wanafunzi wake ilikuwa bado mbali; wanafarakana na Yesu kiroho. Watu wakitaka kumwumiza yesu, na kuambatana na udhalimu wa Mafarisayo, walimgeuzia mgongo, na kumwacha. Wameonyesha uamuzi wao, hawakuandamana na Yesu tena.TVV 217.1

    Maneno ya kweli ya yesu yametenganisha makapi na ngano Mathayo 3:13. maana walijiona kuwa wenye haki, kiasi ambacho hawakukubali kutiwa kasoro. Wengi waliondoka, wakaenda zao. Watu hujaribiwa siku hizi kama wafuasi wa yesu walivyojaribiwa katika sinagogi huko Kapernauamu. Ukweli unaposemwa na kuingia moyoni watu huona makasoro yote waliyo nayo, ila huwa hawakubali kujinyima, huenda zao hali wakichukizwa, na huku wakilalamika, kwamba “Huu ni usemi mzito, nani atausikia”?TVV 217.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents