Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Siri ya kuponywa kiroho

    Mtu huyo lazima alikuwa amepoteza tumaini la kupona. Lakini aliyaamini maneno ya Kristo na alipofuata yale aliyoambiwa alipata baraka ya kupona. Sisi pia tunaweza kupata kuponywa kiroho kwa imani ile ile. Dhambi imetutenga na uzima wa Mungu, na tumekufa ganzi. Hatuwezi kwa nguvu zetu kuishi maisha matakatifu kama mtu yule alivyoshindwa kutembea. Watu wengi wanaotambua kushindwa kwao, nao hujaribu kufaulu kwa nguvu zao hufanya kazi bure. Mwokozi huwainamia watu hao wasumbukao bure, na kusema: “Mwataka kuwa wazima?’ Msingoje kujisikia kuwa mnapona. Yaamini maneno yake na wekeni nia zenu kando ya Kristo. Mkitii maneno yake mtapokea nguvu. Maovu yoyote yaufungao mwili na roho Kristo anaweza kukuokoa. Atatia uzima rohoni, ambayo ni “mfu katika uasi.” Waefeso 2:1TVV 108.3

    Mwenye kupooza aliinama akachukua blanketi yake na virago vyake vingine, alipoinuka akamtafuta Mponyaji wake. Lakini Yesu alikuwa amechanganyika ndani ya mkutano. Alipoondoka akienda zake basi amepona kamili, hali akishangilia kupata nguvu mpya, aliwaeleza Mafarisayo kadhaa juu ya kupona kwake. Alishangazwa na hali yao, jinsi walivyosikiliza habari hizo kwa ubaridi sana.TVV 108.4

    Pole pole walimkata kauli wakimwuliza, kuwa kwa nini anajitwika kitanda siku ya Bwana. Kwa furaha yule mtu aliyokuwa nayo, alisahau kuwa ilikuwa siku ya sabato. Alijibu kishujaa: “Aliyeniponya ndiye aliyeniambia kuwa “jitwike kitanda chako uende.” Walimwuliza kuwa, ni nani aliyefanya haya, lakini yeye hakuweza kusema. Wakuu hawa walitaka thibitisho dhahiri, ili waweze kumhukumu Yesu kuwa ni mvunja Sobato. Hakuvunja Sabato tu, bali amefanya kosa pia la kumwambia mtu yule abebe kitanda siku ya Sabato.TVV 109.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents