Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hukumu Pana Zaidi

  Mawazo ya Yesu yalisafiri kutoka wakati wa kuangamia kwa Yerusalemu na kufikia hukumu pana zaidi.TVV 421.4

  Katika kuharibiwa mji wa Yerusalemu usiotubu aliona mfano wa uharibifu wa mwisho utakaoupata ulimwengu. “Ndipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tufunikeni kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mti mkavu?” Mti mbichi ulikuwa mfano wake yeye mwenyewe, Mwokozi asiye na hatia. Ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi ilimwangukia Mwanawe mpendwa. Basi ni taabu kiasi gani basi, atakayoibeba mwenye dhambi ambaye akidumu katika dhambi? Wasiotubu watapata huzuni ambayo lugha itashindwa kuielezea jinsi yake.TVV 421.5

  Katika umati uliomfuata Mwokozi mpaka Kalwari, walikuwamo wale waliokuwa katika maandamano ya Hosana, wakiwa na matawi ya mitende, wakati alipoingia Yerusalemu kwa shangwe. Sio wachache waliomsifu siku hiyo kwa sababu ilikuwa hoihoi, sasa wanatuna katika kupiga kelele wakisema; “Msulibishe, Msulibishe.” Wakati Kristo alipoingia Yerusalemu kwa shangwe wanafunzi walikuwa wakimsongasonga, wakiona kuwa ni heshima kuambatana naye. Sasa katika kudhalilishwa kwake wanamfuata kwa mbali.TVV 421.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents