Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Msaada Kutoka Sehemu Isiyotazamiwa

  Yusufu alikwenda kwa Pilato kiujasiri akamwomba mwili wa Yesu. Kwa mara ya kwanza, Pilato akajua kuwa Yesu amekwisha kufa. Habari za kifo cha Yesu ziliachwa kuelezwa kwa Pilato kwa makusudi. Alipopata ombi la Yusufu, alimwita yule akida aliyepewa jukumu la ulinzi pale msalabani na akapata maelezo ya mambo na matukio ya Kalivari ili kuthibitisha ushuhuda wa Yusufu. Yusufu akapata ruhusa ya Pilato kuuchukua mwili wa Kristo, na Nikodemo naye akaja na manukato na udi ya thamani yapata ratli mia ili kupaka mwili wa Yesu. Mheshimiwa kushinda wote katika Yerusalemu hangeheshimiwa kiasi hicho katika mazishi yake. Wanafunzi walishangaa sana.TVV 438.5

  Wakati Mwokozi alipokuwa angali hai Yusufu wala Nikodemo hawakujidhihirisha kuwa walimkubali. Hatua kama hiyo ingesababisha watolewe katika Sanhedrini, na wao walitaka kumlinda na mvuto wao. Lakini Wayahudi wenye hila walikwamisha mipango yao. Wakiwa hawapo Yesu alihukumiwa. Sasa Yusufu na Nikodemo hawakuweza tena kuficha uhusiano wao kwake. Sasa wakajitokeza kijasiri kuwasaidia wanafunzi masikini. Kwa taadhima na taratibu kwa mikono yao weyewe wakaushusha mwili wa Yesu kutoka msalabani. Machozi ya huruma yaliwatoka walipoutazama mwili uliochubuliwa na kujeruhiwa. Yusufu alikuwa na kaburi jipya lililochongwa mwambani kwa ajili yake binafsi. Nalo lilikuwa karibu na Kalvari, na sasa akaliandaa kwa ajili ya Yesu. Hapo wale wanafunzi watatu walinyosha viungo vyake, na kuikunjia kifuani mwake mikono iliyochubuliwa na kumweka kaburini. Kisha jiwe zito liliviringishwa na kuwekwa mlangoni mwa kaburi, na Mwokozi kaachwa apumzike.TVV 439.1

  Wakati giza la jioni lilipokuwa linasogea, Mariamu Magdalena na Mariamu wengine walivinjari mahali alipolala Bwana wao wakiwa wanatiririkwa na machozi ya huzuni. “Wakarudi . . . wakastarehe siku ya Sabato kama ilivyoamriwa.” Luka 23:56.TVV 439.2

  Hiyo ilikuwa Sabato isiyoweza kusahaulika kamwe kwa wanafunzi wake, na makuhani, wakuu, waandishi na watu wote. Pasaka iliadhimishwa kama ilivyokuwa ikifanyika kwa karne zote, wakati aliyemwakilisha alikuwa amelala katika kaburi la Yusufu. Viwanja vya hekalu vilijaa watu waliokuja kuabudu. Kuhani mkuu alikuweko pale, akiwa amevalia mavazi yake rasmi. Makuhani wakiwa wenye shughuli nyingi waliendelea kuhudumu. Ingawa hivyo wengine hawakuwa na mapumziko licha ya damu za ng’ombe na mbuzi kwa ajili ya dhambi. Walikuwa hawana habari kuwa mfano ulikuwa umekutana na sadaka halisi, kwamba, Sadaka ya thamani mno ilikuwa imetolewa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote. Lakini kamwe huduma hiyo haikupata kushuhudiwa na hisia zilizopingana hivyo. Hali isiyo kawaida ilitawala kila kitu. Patakatifu mno palipokuwa pakifichwa pasiingiwe, sasa kutokana na pazia kupasuka toka juu mpaka chini, palionekana kwa macho ya watu wote, Bwana alikuwa hapatambui tena. Kule kufunuliwa kwa patakatifu kuliwatia hofu makuhani kwa kutazamia maafa kuwafika.TVV 439.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents