Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  33 — Jinsi Yesu Alivyojihusisha na Matatizo ya Jamaa

  Watoto wa Yusufu walikuwa mbali sana na kazi ya Yesu, wala hawakumhurumia hata kidogo, wala kumsaidia. Habari za maisha yake na kazi yake viliwachukiza. Walisikia kuwa alikuwa akikesha usiku kucha akiomba, na kwamba wakati wa mchana alizungukwa na makutano ya watu, hata hakuwa na nafasi hata ya kupumzika, wala kula. Rafiki zake waliona kuwa atajichakaza mwenyewe kwa jinsi hiyo, wala hawakuweza kugeuza hali yake mbele ya Mafarisayo; na wengine waliona kuwa mambo yake yamezidi.TVV 174.1

  Ndungu zake waliona haya kwa ajili ya mashutumu yatokanayo na hali yake, akiwa jamaa yao. Waliona uchungu sana kwake kwa ajili ya masuto ya Mafarisayo. Lazima atakuwa amekoma kufanya kazi kwa jinsi hiyo. Walimshawishi Mariamu awaunge mkono kumlaumu, wakidhani kuwa upendo wake kwake utafaulu kumgeuza. Mafarisayo wamemlaumu mara nyingi kuwa:” .... Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo” Mathayo 9:34. Kristo aliwaambia kuwa wale wanaompinga hawaelewi na tabia yake ya Uungu; kwa hiyo hawana budi kusamehewa. Kwa Msaada wa Roho Mtakatifu wataona makosa yao na kutubu. Lakini mtu anayekataa kazi ya Roho Mtakatifu hujiweka katika hali ambayo kutubu hakutamfikia. Watu wakimkataa Roho Mtakatifu kwa ukaidi, na kumtaja kuwa ni Shetani, huwa wamekata kiungo cha kuongea na Mungu.TVV 174.2

  Mafarisayo wenyewe hawakuyaamini malaumu waliyomlaumu Yesu. Wakuu hao walisikia sauti ya Roho mioyoni mwao ikiwashuhudia kuwa Yesu ndiye Mpakwa Mafuta wa Israeli. Mbele yake walijitambua kuwa wao si watakatifu, na walitamani haki ya kweli. Lakini baada ya kumkataa, ilionekana kuwa ni kujishusha kukubwa sana kumkubali kuwa ndiye Masihi. Kwa hiyo walishindana na kuyabishia mafundisho ya Mwokozi ili kuepukana na kumkiri kuwa ndiye Masihi. Hawakuweza kumzuia asitenda miujiza, ila walijitahidi kumnena vibaya isivyo haki. Hata hivyo Roho wa Mungu wa kuwakirisha kwamba ni yeye Masihi, ilikuwa kati yao. Lakini wao walijaribu wawezavyo kujenga ukuta wa kutoamini.TVV 174.3

  Mungu hawezi kuwaacha watu wawe vipofu, na kuwafanya kuwa wagumu wa mioyo kiasi cha kutoweza kuona ukweli. Huwatumia nuru ili kuwaangaza waone makosa yao. Lakini wasipojali nuru hiyo macho yao hupofuka na mioyo yao huwa migumu kiasi cha kutatanika. Nuru moja isipojaliwa huleta giza fulani katika hali ya kiroho, na mtataniko wa hali ya kiroho huzidishwa. Giza la kiroho huongezeka, mpaka huwa giza kamili katika roho. Ndivyo ilivyokuwa kwa viongozi wa Mafarisayo katika taifa la Wayahudi. Wakaihesabu kazi ya Roho Mtakatifu kuwa ni kazi ya Shetani. Kwa kufanya hivyo walichagua njia ya udanganyifu, na hivyo wakajitia katika utawala wa Shetani.TVV 175.1

  Maneno yanayokaribiana na onyo la Kristo kuhusu kumtukana Roho Mtakatifu, ni yale ya usemi mbaya. Maneno ndiyo yanayoonyesha tabia ya mtu ilivyo. “Kinywa cha mtu huyanena yale yaujazayo moyo wake.” Maneno yana uwezo wa kuonyesha tabia ya mtu. Mtu hupimwa kwa maneno anenayo. Mara nyingi maneno ya ubishi huongozwa na Shetani, husemwa tu bila kufikiriwa, lakini matokeo huonyesha mambo ya moyoni. Maneno yasemwayo katika utani hupitia hivyo bila kusahihishwa. Husemwa tu kwa namna hiyo.TVV 175.2

  Ni hatari kusema maneno ya mashaka, na kubishia maneno ya kweli, ya nuru. Maneno hafifu na yasiyo na adabu huhusiana na tabia ya mtu, nayo huonyesha mashaka na kutoamini. Mtu huendelea hivyo mpaka mwisho hukanusha hata yaliyo ya kweli. Yesu alisema: “Kila neno lisilo maana watu watakalonena, watatoa hesabu yake siku ya hukumu. Maana kwa maneno yako utapewa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.”TVV 175.3

  Kisha Yesu alitoa onyo kwa wale walioguswa na maneno yake, lakini hawakuchukua hatua yoyote. Pepo mchafu akimtoka mtu, huenda huko na huko, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Kisha husema, Nitarudi katika nyumba yangu ya zamani nilikotoka. Hurudi huko na kuikuta nyumba yako safi imefagiliwa. Halafu huchukua mashetani wengine saba walio waovu kuliko yeye nao huingia na kuishi humo.”TVV 175.4

  Wengi katika siku za Kristo, kama walivyo leo, huwekwa huru kwa neema ya Mungu, kutokana na nguvu za mwovu. Hufurahia upendo wa Mungu, kwamba Kristo atakaa ndani yao. Wakati roho wa mashetani akiwarudia pamoja na wengine saba walio waovu kuliko yeye, basi hutawaliwa na roho ya mashetani.TVV 176.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents