Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Yesu alijali

  Wanafunzi wakishughulika katika kujitahidi kujiokoa, walisahau kuwa Yesu alikuwamo mashuani. Sasa wakiona kuwa kifo kinawajia, walimkumbuka yule ambaye ndiye wokovu wao, ambaye ndiye aliyewaagiza kuvuka ng’ambo ya ziwa. Yeye ndilo tumaini lao tu. Wakaita: Bwana, Bwana! Lakini sauti zao zilififia kwa ajili ya ngurumo kuu ya tufani, na hawakusikia mtu akiwajibu. Wakashikwa na hofu na wasiwasi sana. Je, huyu anayefukuza pepo na magonjwa, hata na kifo, hana uwezo iuu ya tufani hii yenye hatari, wala hawezi kuwaokoa wanafunzi wake katika balaa hili? Je, ni kusema kuwa haiali?TVV 184.1

  Mara tena waliita, bila kujibiwa, ila tu ngurumo ya tufani. Ilivyoonekana ni kuwa wataangamia katika maji.TVV 184.2

  Ghafla umeme ukamulika katika giza, wakamwona Yesu akilala kwa utulivu, wala hana wasiwasi na kelele za tufani. Kwa mshangao wakasema: “Bwana, huom kuwa tuko katika kuangamia?”TVV 184.3

  Sauti za kilio chao zilimwamsha Yesu. Umeme ulipomulika walimwona, akiwa na utulivu wa mbinguni katika uso wake, na utulivu wa upendo ulionekana kwake, ndipo wakasema: “Bwana, tuokoe tunaangamia.TVV 184.4

  Hakuna kilio cha moyoni kilitolewa kisijibiwe kamwe. Wanafunzi waliposhika makasia yao kujaribu tena kuiisogeza, Yesu alisimama. Tufani ilipozidi hata kuwamwagia maji, aliinua mkono wake, akasema kwa bahari yenye fujo, “Tulia”.TVV 184.5

  Mawimbi yalizama, mawingu mazito yalitoweka, na nyota zikaonekana ziking’aa. Mashua ikatulia juu ya maji ya bahari. Kisha Yesu aliuliza swali kwa masikitiko, “Mbona mliogopa? Hamna imani”? Wanafunzi wakawa kimya. Hofu na aibu ikawashika wenye mashua waliofuatana na Yesu. Tufani ilikuwa imeisukuma mashua karibu na pwani, na wote waliokuwemo mashuani waliona kuwa ni mwujiza. Watu wakanong’onezana, “Huyu ni mtu wa namna gani, hata upepo na bahari humtii?”TVV 184.6

  Yesu alipoamka kukabiliana na dhoruba, hakuwa na alama ya hofu, wala hakuwa na alama ya wasiwasi kwake. Lakini hakuwa katika mikono ya Mwenyezi. Hakuwa Bwana wa nchi na bahari na mbingu, aliyepumzika kwa utulivu Uwezo huo aliuacha. “Siwezi kufanya kufanya neno mwenyewe.” Yohana 5:30. Alitegemea uwezo wa Baba Ilikuwa imani, imani kwa Mungu na upendo wake na uangalizi wake. Hapo ndipo Yesu alitulia. Uwezo wa neno lililotuliza bahari na dhoruba ulikuwa uwezo wa Mungu.TVV 184.7

  Vivyo hivyo na sisi yatulazimu kuegemea kwa uwezo wa Mwokozi wetu. Hofu ya wanafunzi ilitokana na kutokuwa na imani, walimsahau Yesu, na wakati walipomrudia na kumkumbuka, ndipo aliwasaidia.TVV 185.1

  Ni mara ngapi wakati tufani ya majaribu inapotukusanyikia hupigana nayo tukiwa peke yetu? Huzitegemea nguvu zetu mpaka tunapokuwa tayari kupotea, ndipo humkumbuka Yesu. Tunapomwita ili atuokoe, mwito wetu hauwezi kuwa kitu cha bure. Hawezi kushindwa kutupa msaada tunaouhitaji. Tunapokuwa na Mwokozi katika roho zetu, hatuwezi kuhofu kitu. Mwokozi atatutoa hatarini kwa njia anayoona kuwa inafaa.TVV 185.2

  Wokovu ni kama bahari iliyochafuka. soma Isaya 57:20. Dhambi imeharibu amani yetu. Tamaa mbaya katika roho zetu hakuna uwezo wa kibinadamu unaoweza kuzitawala. Hatuwezi kufanya chochote ili kuzishinda Ni sawa na wanalunzi walipokuwa wakisshindana na dhoruba, bila matumaini yoyote. Walakini hata kama tufam ya majaribu ni kubwa kiasi gani, wale wanaomlilia Yesu kwamba: “Bwana, tuokoe” watapata ukombozi Neema yake hunyamazisha tamaa zote, na katika upendo wake roho zetu hupumzika kwa utulivu. “Hutuliza dhoruba, ikiwa shwari, mawimbi yake yakanyamaza. Ndipo walipofurahi kwa kuwa yametulia, Zaburi 107:2930.” “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia va Bwana wetu Yesu Kristo.” Warumi 5:1.TVV 185.3

  Asubuhi na mapema mwokozi na rafiki zake, walilika Pwani. Miali ya jua ikamulika na kuleta uhai duniani Wahpofika pwam waliona kitu cha kutisha kuliko dhoruba ya usiku. Wenda wazimu wawili waliwakimbilia kana kwamba wanataka kuwararulia mbali. Watu hawa walikuwa na vipande vya minyororo vikining’inia mikononi mwao ambavyo walifungwa navyo, nao wamevikatia mbali. Miili yao ilikuwa imekatwa katwa, na ilikuwa ikitoka damu. Walikuwa wamekodoa macho yao, karibu kutoka mahali pake. Nywele zao zilikuwa matimutimu. Walikuwa na roho za mashetani, nao walionekana katika hali ya kutisha sana, kama wanyama wa mwituni wala si kama watu.TVV 185.4

  Wanafunzi walikimbia kwa hofu iliyowapata; lakini wao walimkabili Yesu. Yeye alikuwa akisimama pale wanafunzi wake walipomwacha. Yeye aliyetuliza dhoruba hakukimbia. Watu wale walikuwa wakitoa povu midomoni, nao walimkabili Yesu. Kristo aliinua mkono ule ulioituliza dhoruba, na watu wale walisimama kitambo kidogo kutoka kwa Yesu. Kwa uwezo mkuu, yesu aliwaamuru mashetani wale watoke ndani ya watu hao. Maneno yake yalipenya mpaka katika akili za watu hao, ambazo zilikuwa zimevurugwa vibaya na mashetani. Walitambua kuwa yuko mtu awezaye kuwafungua kutoka katika janga hili la mashetani. Lakini walipofungua vinywa vyao ili kuomba msaada, mashetani ndio walisema ndani yao, nao walisema kwa nguvu: “Tuna nini nawe Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese.TVV 185.5

  Yesu aliuliza, “Jina lako nani?” Jibu likaja: “Jina langu ni Legion, maana tu wengi.” Mashetani walimsihi Yesu asiwatoe nchini. Kando ya mlima kulikuwako na kundi la nguruwe likijilisha. Mashetani walimwomba Yesu awaruhusu wawaingilie. Kwa ghafla kundi lote likakimbia kiwazimu mpaka ziwasni wakafa majini.TVV 186.1

  Mara moja mabadiliko yalitokea lwa watu waliokuwa wenye kichaa. Nuru ya kweli imemulika katika akili zao.Wakaona kama wenye akili kamili. Wakamtukuza Mungu kwa kuponywa kwao.TVV 186.2

  Kule gengeni walisha nguruwe waliona yote yaliyotokea, kwa hiyo wakakimbia mjini kueleza habari hizi kwa wenye nguruwe. Kwa hofu na kwa mshangao mji wote ukatoka kumjia Yesu. Wenye wazimu hao walikuwa tishio katika nchi. Hakuna mtu aliyepita mahali pao kwa usalama. Sasa watu hawa wamepona, wanamsikiliza Yesu, na kumtukuza Mungu kwa furaha. Kupotea kwa nguruwe kulionekana kuwa ni jambo muhimu kuliko kuponywa kwa watu hawa.TVV 186.3

  Wenye nguruwe walikuwa wakitaka mali za ddunia tu kuliko mali ya mbinguni. Yesu alitaka kuvunja choyo na upendo wa mali ili waweze kusikiliza maneno yake yenye uzima.TVV 186.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents