Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kile Kinachotuchosha

    Watu wengi wenye kuelemewa na mizigo ya masumbufu ya kila namna, huwa wanafanya kazi ya ulimwengu na kukubaliana na kanuni zake na njia zake. Hivyo maisha yao huwa ya matatizo tu wakati wote. Kwa kutamani mambo ya ulimwengu, hujeruhi hali zao, na kujiletea mizigo isiyo ya lazima; ambayo ni mizigo ya matatizo tu. Bwana wetu hutaka waondoe mizigo hii, ambayo ni kongwa la utumwa. Husema: “Nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.” Huwashauri kutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake. Wasiwasi ni kipofu hauwezi kutambua mambo ya wakati ujao. Lakini kwa kila tatizo Yesu huwa ameandaa njia tayari ya unafuu. Baba yetu wa mbinguni anazo njia maelfu za kutusaidia; ambazo sisi hatuzijui. Wale wanaoifanya kazi ya Mungu na heshima yake kuwa kitu cha kwanza, wataona kuwa wasiwasi wao umetoweka, na kuna njia wazi safi iko mbele yao.TVV 180.4

    “Jifunzeni kwangu.” Huo ndio usemi wa Yesu. Kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha.” Tunapaswa kuingia katika skuli ya Kristo na kujifunza kwake. Wokovu ni mfululizo wa kujifunza mambo ya mbinguni; yaani mambo ya kiroho. Mafundisho haya ni kujikabidhi kwa Kristo kamili, kimawazo, kimazoea na kimatendo; yaani kuachana na kanuni za giza, ambazo huongozwa na Shetani.TVV 180.5

    Moyoni mwa Kristo kulikuwa na amani kamili. Hakupotoshwa na kusifiwa wala kudharauliwa. Kunenwa vema au kunenwa vibaya. Kutendwa vema au kutendwa vibaya. Katika mambo hayo yote, Yesu alikuwa na hali ile ile. Lakini wengi wa wafuasi wake huwa na hali ya wasiwasi na msukosuko moyoni, kwa sababu huogopa kumtegemea Mungu. Huwayawaya kwani hawajitoi kamili kwa Mungu. Walakini wasipojitoa kamili kwa Mungu hawawezi kupata utulivu na amani kamili.TVV 181.1

    Wakati tunapozaliwa kutoka juu, tutakuwa na nia ile ile iliyokuwa kwa Yesu. Ndipo hatutatafuta vyeo vya juu. Tutatamani kuketi miguuni mwa Yesu, na kujifunza kwake. Tutafahamu kuwa thamani ya kazi yetu, ni kadiri ya kumwagiza Roho Mtakatifu kwetu. Kumtegemea Mungu huleta utakatifu katika nia, ili kwamba katika uvumilivu tuokoe roho zetu.TVV 181.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents