Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hakuna udhuru kwa majaribu

    Majaribu ya Shetani hayawezi kufanyiwa udhuru. Hakuna udhuru kwa kutenda dhambi. Kila mtoto wa Mungu mwenye kutubu, lazima achuchumilie kuwa na hali ya kufanana na mtoto wa Mungu, akijivika hali ya hasira njema katika mambo yote.TVV 167.4

    Yesu aliishi maisha makamilifu alipokuwa hapa duniani kama mwanadamu, hivyo wafuasi wake nao wapaswa kuwa kama alivyokuwa. Yesu alifananishwa na ndugu zake katika mambo yote. Alikuwa na hali ya namna ilivyo kwetu sisi. Alishiriki mambo yetu ya kibinadamu, walakini bila kasoro yoyote. Alikuwa Mungu katika mwili, akiwa na tabia kama zetu. Kristo ndiye ile ngazi Yokobo aliyoiona katika ndoto ambayo kitako kilifika chini, na kilele chake kikifika juu mbinguni. Kama ngazi hiyo ingalishindwa kufika chini, tungalipotea. Lakini Kristo alitufikia mahali tulipo. Alitwaa hali yetu, akashinda, ili sisi tukitwaa hali yake tushinde pia. Akafanywa kuwa “mwili wa dhambi” (Warumi 8:3) lakini akaishi bila dhambi. Sasa anatuagiza kwa njia ya imani, tushike utukufu wa tabia ya Mungu, twapasa kuwa “wakamilifu kama Baba aliye mbinguni alivyo mkamilifu.”TVV 167.5

    Yesu alikuwa ameonyesha kile ambacho ndiyo haki na alikuwa ameonyesha kuwa Mungu ndiye asili ya haki. Sasa aligeukia upande wa wajibu na shughuli zipasazo haki. Kitu cho chote kisifanyike chenye kuleta mvuto wa ubinafsi. Wasaidie maskini kwa stahili yao, wala si kujivutia hali ya ubinafsi, yaani kukusifu wewe. Katika maombi, zungumza na Mungu. Katika kufunga usiwe na roho ya kujionyesa kuwa wewe ni mtawa, umefunga, huo ni ubinafsi.TVV 168.1

    Huduma yo yote inayotendwa bila kuwa na ubinafsi ndani huwa na sifa kubwa mbele za Mungu. “Baba yenu wa mbinguni atakujaza kwa dhahiri.” Katika maisha yetu tuishiyo tabia zetu hujengeka kwa neema ya Kristo. Hali ya Ukristo wa Yesu hupatikana ndani yetu, na sura ya Mungu huanza kuonekana kwetu. Watu wanaoenenda na kutenda kazi pamoja na Mungu hali ya mbinguni huwazunguka. Watu hawa ufalme wa Mungu umeanza ndani yao.TVV 168.2

    “Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili.” Dini ya Biblia haina mivuto mingi katika mchanganyiko; inaingia katika sehemu zote za maisha.TVV 168.3

    “Jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa nuru lakini jicho lako likiwa ovu, mwili wako wote utakuwa giza.” Anayetamani kuijua kweli lazima awe tayari kuikubali kweli yote inayofunuliwa kwake. Kutangatanga na kushika kweli nusu nusu ni kuchagua njia ya makosa ni udanganyifu wa Shetani.TVV 168.4

    Kanuni za ulimwengu na kanuni za dini ya Mungu haziafikiani hata kidogo; ni kama rangi za upindi wa mvua. Kati ya kanuni hizo mbili, kanuni ya Mungu ni dhahiri kabisa. Sura ya Kristo hutofautiana na ya Shetani. Kanuni hizo hutofautiana kama mchana na usiku. Watu wale wanaoishi maisha ya Kristo, ndio watu wake.TVV 168.5

    Wote waliochagua kazi ya Mungu hustarehe katika ulinzi wake. Kristo alitaja juu ya ndege warukao na maua yaotayo na kusema: “Ninyi je, si bora kuliko vitu hivyo?” Ndege wadogo kama shorwe hutunzwa. Maua na majani hutunzwa na kulindwa na Baba wa mbinguni. Mwenyezi, ambaye ni Muumbaji, hujishughulisha na mambo madogo kama haya, na kuyafanya yatoe maua kama ya Sulemani. Je atamtunza mtu kiasi gani, ambaye alimwumba kwa sura yake, na utukufu wake. Kama vile jua hutoa nuru yake na kuing’azia maua madogo, ndivyo Mungu hutoa uzuri wake na kuwang’arizia watu, na kuwapa tabia yake.TVV 168.6

    Katika kitabu cha Mungu, maisha tunayoishi huwa na ukurasa wake wa pekee. Katika ukurasa huo huandikwa kila jambo la maisha yetu yote. Jambo kwa jambo, kubwa au dogo. Wana wa Mungu hawawezi kusahauliwa hata katika mawazo yake. “Kwa hiyo msisumbukie mambo ya kesho.” Mungu hakuwafunulia watoto wake mambo yote ya maisha ya safari yao. Huwambia yale wanayoweza kukumbuka na kufanya. Yale wanayofunuliwa huhusu wakati huo tu.TVV 169.1

    “Msihukumu msije mkahukumiwa.” Msijidhanie kuwa ninyi ni bora kuliko watu wengine, na kujifanya mahakimu wao. Hamwezi kuona makusudi ya matendo yao. Katika kuwalaumu, huwahukumu. Kwa njia hiyo hujiunga na Shetani; ambaye ni mshitaki wa ndugu. Tazama 2 Wakorintho 13:5; 1 Wakorintho 11:31.TVV 169.2

    Mti mwema huzaa matunda yaliyo mema. Vivyo hivyo matunda yanayozaliwa katika maisha hudhihirisha tabia ya mtu. Matendo mema hayawezi kununua wokovu, lakini huonyesha kuwa kuna imani ifanyayo kazi kwa upendo, nayo hutakasa moyo. Zawadi haitolewi kwa ajili ya kazi bora tuliyofanya, walakini kwa kadiri ya kazi ya uaminifu iliyofanywa kwa neema ya Mungu.TVV 169.3

    Kristo aliweka kanuni ya ufalme wake. Ili kukaza’ kufundisha aliongeza kielelezo. Haitoshi kusikiliza tu maneno yangu, kwa kuyatii mtayafanya kuwa asili ya tabia zenu. Mkijenga juu ya hadithi za wanadamu, nyumba zenu zitaanguka. Zitaangushwa na upepo wa majaribu, na matatizo vitazibomolea mbali. Lakini kanuni hii niliyowaonyesha itadumu, na nyumba zenu hazitaanguka. Nikuba lini, jengeni katika maneno yangu.TVV 169.4

    “Kila mtu asikiaye maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake katika mwamba; mvua ikanyesha mafuriko yakaja, pepo zikavuma zikaipiga nyumba hiyo isianguke, kwa sababu misingi yake imewekwa katika mwamba.”TVV 169.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents