Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Imani ya Mariamu yapata thawabu

  Ingawa Mariamu hakufahamu vizuri kazi ya Kristo, alimtegemea. Kwa hiyo Yesu alikubali imani hii kwa ajili ya kuheshimu imani yake na kwa ajili ya kuimarisha imani ya wanafunzi wake, alifanya mwujiza wa kwanza. Kwa wanafunzi ilidhihirika kabisa kuwa yeye ni Masihi, lakini walisikitika sana kwa kutoamini kwa makuhani na walimu wa Kiyahudi kwamba Yesu ndiye Masihi. Mwujiza huu uliwaimarisha wanafunzi wake katika mashindano yao ya upinzani.TVV 76.1

  Mariamu aliwaambia waliokuwa wakihudumu katika meza, “Lolote atakalowaambia, lifanyeni.”TVV 76.2

  Kando ya mlango kulikuwako na mabalasi makubwa sita Yesu aliwaambia watumishi wayajaze maji. Kisha akasema, “Choteni sasa maji hayo mkampelekee mkuu wa karamu.” Badala ya kuwa maji tu, yakageuka kuwa divai tamu.TVV 76.3

  Walipoyaonja maji hayo yaliyoletwa na watumishi, mkuu wa karamu akaona kuwa ni matamu kuliko yote aliyopata kunywa. Akimgeukia mkuu wa meza, alisema, “Kila mtu hutanguliza kuleta divai nzuri, na watu wakisha kushiba, huleta ile mbaya, lakini wewe umengoja na divai nzuri mpaka sasa.TVV 76.4

  Zawadi zinazotolewa na ulimwengu zinaweza kupendeza macho na kuleta utamu, lakini hazitoshelezi chochote. Mvinyo hugeuka kuwa uchungu, shangwe hugeuka kuwa majonzi, kilichoanza kwa shangwe na furaha huishia katika uchungu na ghasia. Bali zawadi ya Yesu ni ya kudumu daima. Karamu anayoandaa ni ya kudumu, na huleta furaha. Hakuna upungufu wowote. Kama ukiishi ndani yake, zawadi nzuri ya leo, hukukaribisha katika zawadi bora ya kesho.TVV 76.5

  Zawadi ya Kristo katika arusi, ilikuwa mfano tu. Maji yaliyojaza mabalasi yaliletwa na wanadamu, lakini Neno la Mungu peke yake ndilo liliweza kutia uhai na ladha. Neno la Kristo lilitoa ladha ya kuwaridhisha watu karamuni. Hivyo wingi wake ndio unaondoa udhalimu na kusafisha moyo. Divai iliyofanywa na Yesu karamuni na ile aliyowapa wanafunzi, ambayo ilikuwa mfano wa haya Isaya husema, wakati akitaja divai mpya: “Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, “Usikiharibu, maana mna baraka ndani yake. Isaya 65:8.TVV 76.6

  Kristo alionya katika Agano la Kale, akisema: “Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; akosaye juu ya hayo hana hekima” Mithali 20:1. Yesu kamwe hakufanya kitu kama hicho. Shetani huwapa kitu kama hicho ili kuvuruga akili zao na kupumbazika wasiweze kupambanua kitu. Lakini Kristo hufundisha kuwa inatubidi tuvitiishe viungo vyetu ndani ya amri. Yesu ndiye alifundisha kwamba Yohana Mbatizaji asinywe mvinyo wala kileo chochote. Alisema mambo hayo kwa mke wa Manoa, mamaye Samsoni. Naye alilaam mtu ambaye atampa jirani yake kileo. Kristo hakukanusha mafundisho yake. Divai aliyofanya katika karamu ya arusi ni matunda yasiyochacha ya mzabibu.TVV 76.7

  Wageni walipokunywa walitaharuki, na kuulizauliza habari za divai hii tamu, watumishi waliwaeleza kuwa huu ni mwujiza. Makutano walipomtafuta Yesu, alikuwa ameenda zake.TVV 77.1

  Sasa waliwageukia wanafunzi, waliokuwa na nafasi ya kuonyesha imaru yao kwa Yesu. Walisema mambo waliyoona na kusikia juu ya Kristo, kule kando ya mto wa Yordani. Habari ya mwujiza huo ilifika mpaka Yerusalemu. Makuhani na wazee wakaamka kwa upinzani kuchungua unabii unaohusu kuja kwa Mashihi.TVV 77.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents