Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  39 — “Wapeni Ninyi Chakula”

  Wanafunzi wa Yesu walifikiri kuwa hawatavurugwa na mtu yeyote, lakini wakati makutano walipomkosa Mwalimu wa mbinguni mda huo, walianza kuulizana: Amekwenda wapi?” Baadhi yao waliona upande alikoelekea pamoja na wanafunzi wke. Watu wengi walikwenda upande huo, wakitembea kwa miguu, na wengine katika mashua ili kumtafuta. Pasaka ilikuwa karibu, na wasafiri wa kwenda Yesusalem, walikuwa na hamu ya kumwona yesu. Watu wengi walikusanyika kiasi cha wanaume 5,000, mbali ya wanawake na watoto.TVV 202.1

  Kutoka kando ya mlima Yesu aliwaangalia makutano waliokusanyika, akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Akiachilia mbali shughuli yake kwa wanafunzi wake, alitafuta mahali pafaapo ili apate kuwahudumia.TVV 202.2

  Watu wakalisikiliza neno la neema kutoka kwa Mwana wa mungu, neno ambalo ni faraja katika mioyo yao. Mikono yenye kuponya ya Kimungu, iliwahuisha wenye dhiki, na wenye maradhi ya kila aina. Siku ilipita kama kivuli, hata wakasahau wakati wa mwisho walipokula chakula.TVV 202.3

  Wakati jua lilipokuwa likichwa wa walikuwa bado wanamzunguka. Yesu alikuwa ameshughulika siku nzima bila pumziko, wala kula; walakini asingeliweza kuwaacha watu wakimzunguka hivyo.TVV 202.4

  Mwisho wanafunzi wake walisema kuwa, ni afadhali watu wawapishe ili nao wapate kula. Watu wengi walikuwa hawajala chochote tangu asubuhi. Katika vijiji na miji inayowazunguka wanaweza kununua chakula wapeni ninyi chakula.” Yesu akimgeukia Filipo, aliuliza: “Tutanunua wapi chakula cha kuwalisha watu hawa? Aliyasema haya ili kujaribu imani ya wanafunzi. Filipo akatazama utitiri wa watu, akasema: “Mikate ya dinari*‘Dinara ni sawasawa na malipo ya siku, kwa kima cha chini. Angalia Mathayo: 1,2 mia mbili haitatosha kila mtu apate kipande kidogo tu.”TVV 202.5

  Yesu akauliza kuwa wanacho chakula kiasi gani. Andrea akasema: “Yuko kijana hapa ana mikate mitano na samaki wawili; na hivi vinafaa nini kwa makutano haya?” Yesu akaagiza wamletee vitu hivi, na wanafunzi wawaketishe watu makundi makundi ya hamsini na mia mia, ili wote washuhudie atakavyofanya. Mambo haya yalipokwisha kutendeka, yesu akatazama mbinguni, akavibariki, na kuvivunja vipande vipande, akawapa wanafunzi wawagawie watu, na akagawanya samaki wawili kwa watu wote. Wakala waote wakashiba. Wakakusanya makapu kumi na mawili ya vipande vya mikate na samaki vilivyobaki. Aliyekuwa akifundisha watu kuwa na amani na furaha alikuwa na uangalifu pia kwa mambo ya kawaida, ya mahitaji yao ya kila siku, kama mambo ya kiroho pia.TVV 203.1

  Kristo kamwe hakufanya miujiza, isipokuwa ilikuwa ni kwa kuimarisha mambo ya lazima tu, na hata hivyo kila mwujiza aliofanya ulikuwa ni kuwapeleka watu kwenye mti wa uzima. Chakula chepesi kilichotolewa na wanafunzi kwa makutano kilikuwa kimejaa mafunisho ya thamani. Maandalizi mepesi yaliandaliwa, ambayo ni samaki wawili na mikate mitano vilivyokuwa chakula cha kuliwa kila siku na wavuvi.TVV 203.2

  Kristo angeweza kuwaandalia chakula kilichokuwa bora zaidi, lakini chakula kinachotolewa ili kutimiza uchu na hamu ya wwatu tu, hakingeweza kutoa fundisho lolote kwa binadamu. Watu haawajafurahia karamu nzuri sawa sawa na watu wale walivyofurahia karamu hiyo iliyotolewa kwao na Kristo, kutokana na chakula chepesi jinsi hiyo.TVV 203.3

  Kama watu wangekuwa na mazoea ya kufanya mambo rahisi na mepesi leo, wakiishi kufuatana na sheria za asili, kungelikuwa na vitu vya kuwatosheleza wa wote, bila wengine kukosa chochote. Kungalikuwa na uhaba wa vitu vichance mno, ambao ni wa kukisia tu kimawazo. Lakini ubinafsi na choyo vimeleta dhambi na umaskini ulimwenguni. Kwa kutano kubwa namna hiyo njaa na uchovu wao, chukula chepesi hicho hakikuwaonyesha uwezo wa utunzaji wake kwa watu wote katika maisha yao. Mwokozi hakuwaahidi wafuasi wake kupata anasa na sikukuu. Chakula chao kinaweza kuwa chepesi tu; haIi yao inaweza kuwa ya kumasikini. Lakini neno lake lasema kuwa, chakula chao hakitakoma, na haja zao zitatimizwa siku zote. Ameahidi kuwa, zaidi ya yote yeye atawafariji kwa kuwako kwake yeye mwenyewe kwao.TVV 203.4

  Katika mavuno ya nchi, Mungu hufanya miujiza kila siku. Kutokana na mambo ya asili na uwezo wake, hutendeka mambo sawa na yale ya kuwalisha makutano. Watu hulima na kupanda mbegu, lakini uzima wa Mungu huzimeesha. Ni Mungu anayewalisha watu mamilioni kila siku kwa njia ya mavumo ya mashambani. Watu wamepewa kazi ya kuendeleza uwezo wake katika mamo ya asili. Mtu hutukuzwa mahali pa Mungu, na vipaji vyake vya thamani hugeuka kuwa laana badala ya mibaraka. Mungu ataka tumtambue kwa ajili ya vipaji vyake. Kufikilisha jambo hili, miujiza ya Kristo ili fanyika.TVV 204.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents