Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jitihada Dhati Kutaka Kumhukumu Yesu

    Mara tu kulipopambazuka Sanhedrini ilikutana, tena na Yesu kwa mara nyingine aliletwa mbele yao. Alikuwa amesema kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, lakini hawakuweza kumtia hatiani kwa jambo hili, kwa sababu Yesu aliposema hivyo ilikuwa wakati wa usiku na watu wengi hawakuwepo na hivyo hawakuwa wamesikia maneno yake. Na walijua kuwa Warumi hawawezi kuona hilo kuwa ni kosa linalostahili adhabu ya kifo. Lakini watu wengi wakisikia wazi akisema kuwa yeye ni Masihi, wangeatafsiri hilo kuwa ni kosa la uchochezi dhidi ya serikali.TVV 401.1

    Wakasema, “Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie.” Lakini Kristo alinyamaza kimya. Wakakazana kumwuliza, maswali. Hatimaye akajibu, “Nijapowa-ambia, hamtasadiki kabisa, tena, nikiwauliza, hamtajibu, wala hamtaniachia.” Lakini akaongeza onyo la dhati, “Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenyezi.” Wakasema, wote “Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu?” “Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye. Wakasema, “Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.” Sasa Yesu alipaswa kuuawa. Kilichokuwa kimebaki kukamilisha ni kwa warumi kuthibitisha hukumu hii.TVV 401.2

    Ndipo ikafuata awamu ya tatu ya kumdhihaki mbaya zaidi, kuliko ile aliyofanyiwa mara ya kwanza. Dhihaka hizi zilitendeka mbele ya makuhani na watawala kwa ruhusa yao. Mahakimu walipotangaza kuwa Yesu atakufa, watu waliingiwa na wazimu wa kishetani. Watu walimrukia Yesu, na kama askari wa Warumi wasingaliwazuia, wangalimpasua vipande vipande kabla ya kufika msalabani. Warumi waliwazuia umati wa watu kwa nguvu wasimdhuru Yesu. Watu washenzi walichukizwa na ukatili aliotendewa mtu ambaye hakupatikana na hatia yo yote. Maofisa wa Warumi walisema kuwa ilikuwa kinyume cha sheria ya Wayahudi kumhukumu mtu kwa ushahidi wake mwenyewe. Jambo hili lilituliza fujo kidogo; lakini viongozi wa Kiyahudi walishikamana bila huruma wala aibu.TVV 401.3

    Makuhani na wakuu walisahau heshima ya vyeo vyao, na wakamdhihaki Mwana wa Mungu kwa sifa mbaya wakimtukania ukoo wake. Walidai kule kujitangaza kuwa Masihi kulimfanya astahili kifo kibaya mno. Walimvika vazi kuukuu kichwani na wakampiga wakisema “Ewe Kristto, tufumbulie; ni nani alikupiga.” Mshenzi mmoja akamtemea mate usoni.TVV 401.4

    Malaika waliandika kila dhihaka, neno na tendo waliyomtendea Jemadari wao mpendwa. Siku moja hawa watu duni walioudhihaki uso mtulivu na wa majonzi wa Yesu, watautazama utukufu wake, uking’aa kuliko jua.TVV 402.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents