Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Malaika Wangalifurahi Kumwokoa Kristo

  Malaika wa mbinguni walitamani kumwokoa Kristo. Kama ingalilazimu kumwokoa, wangaliharakisha kumwondoa kwa upesi gani kiasi katika fedheha hiyo, na kuwaangamiza maadui hao wa Mungu! Lakini waliagizwa wasifanye hivyo. Maana ilikuwa ni sehemu ya kazi yake ya ukombozi kupitia katika fedheha zote hizo, kadiri ambavyo wanadamu wangemtwisha.TVV 395.1

  Kristo hakusema lo lote kuwapa mwanya waliomshitaki, lakini hata hivyo alifungwa kuonyesha kuwa alikuwa amehukumiwa. Lakini hata hivyo, sharti uwepo mfano wa kusikiliza kesi kisheria. Hilo watawala walikusudia kuharakisha: Walijua watu walivyompenda Yesu, na kuhofia kuwa wangejaribu kumwokoa. Na pia, kama wangekawia kutekeleza hukumu, mara moja, wangalipaswa kungojea kwa juma moja kwa sababu ya Pasaka. Mambo haya yangaliharibu mipango yao. Kama wangalingojea juma jingine, kungetokea upinzani. Wangalitokea mashahidi wengine wenye ushuhuda kuonyesha hana hatia na kudhihirisha matendo makuu aliyotenda Mashitaka ya Sanhedrin yangalikosolewa na Yesu angalifunguliwa. Kwa hiyo Makuhani na wakuu waliazimia kuwa kabla ya kugundulika. kusudi lao, Yesu lazima atiwe mikononi mwa Warumi.TVV 395.2

  Lakini kwanza, shitaka lazima lipatikane. Mpaka hapo walikuwa hawajapata la kumshitaki. Anasi aliagiza Yesu apelekwe kwa Kayafa. Ingawa hakuwa na tabia nzuri Kayafa alikuwa mkatili na mbaya kama Anasi. Ulikuwa sasa mapambazuko, na bado giza wakati kundi lenye silaha pamoja na mahabusi walipokwenda: kwa kuhani mkuu. Wakati Sanhedrini likikusanyika, Anasi na Kayafa kwa mara nyingine walimhoji Yesu maswali bila mafanikio.TVV 395.3

  Ndani ya jumba la mahakama Kayafa alikalia kiti. Katika upande walikaa wahukumu na wasikilizaji wah usika. Askari wa Kirumi waliketi juu ya jukwaa chini ya kiti cha hukumu. Yesu alisimama mbele ya kiti cha enzi. Hali ilikithiri sana. Yesu peke yake ndiye aliyekuwa kimya na mmtulivu.TVV 395.4

  Kayafa alikuwa akimuona Yesu kuwa ni mpinzani wake. Ile hamu ya watu ya kutaka kusikia mafundisho ya Mwokozi, ilichochea wivu wa kuhani mkuu juu ya Yesu. Lakini sasa Kayafa alipomtazama mshitakiwa aliguswa na hali yake ya heshima na utukufu. Akakiri wazi kuwa mtu huyu ni mwenye asili ya Uungu, Kwa muda uliofuata wazo likatoweka, na kwa kejeli akamtaka Yesu atende mojawapo ya miujiza yake mikuu. Lakini maneno yake yalianguka masikioni pa Mwokozi kana kwamba hakuyasikia. Katika mawazo ya watu hawa wakaidi swali likajitokeza, Je! huyu mtu mwenye mwonekano wa Uungu ahukumiwe kama mhalifu?TVV 395.5

  Maadui wa Yesu walipigwa butwaa. Jinsi ya kukamilisha hukumu yake hawakujua. Kayafa alitaka kujiepusha na kuanzisha ubishi. Kulikuwa na mashahidi wengi wa kuthibitisha kuwa Yesu aliwaita makuhani na waandishi kuwa ni wanafiki na wauaji lakini haya yasingefaa kwa wakati huu. Ushahidi kama huo haungekuwa na nguvu mbele ya serikali ya Kirumi. Kulikuwa na ushahidi mwingi kuwa Yesu alidharau mambo mengi kuhusu kanuni za Wayahudi. Ushahidi kama huo pia usingekuwa na nguvu mbele ya serikali ya Kirumi. Maadui wa Kristo hawakuthubutu kumshitaki na uvunjaji wa Sabato, kusudi mahojiano yake yasije yakaweka wazi miujiza yake ya kuponya.TVV 396.1

  Mashahidi wa uongo walikuwa wamenunuliwa ili kutoa ushahidi kuwa Yesu alikuwa na mpango wa kuanzisha serikali nyingine. Lakini ushahidi wao haukuwa dhahiri, na ulipingana. Walipohojiwa walisema uongo.TVV 396.2

  Mwanzoni mwa kazi yake, Kristo alisema: “Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.” Hivyo alikuwa akitabiri juu ya kifo chake, na ufufuo. “Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.” Yohana 2:19, 21. Lakini katika mambo yote Kristo aliyosema, makuhani hawakuweza kupata kitu cho chote cha kumkandamizia, isipokuwa hili. Warumi walikuwa wamelijenga upya na kulipamba hekalu na hivyo walilijivunia, hivyo dalili yo yote iliyoonyeshwa juu yake, ingeamsha hasira yao. Katika hilo Warumi na Wayahudi walikubaliana; kwa sababu wote walilitukuza sana. Wali-shirikiana katika kuliheshimu.TVV 396.3

  Shahidi mmoja aliyenunuliwa kumshtaki Yesu. Akasema, “Mtu huyu alisema kuwa atalivunja hekalu hili la Mungu, na kulijenga katika siku tatu.” Kama maneno ya Yesu yalingalinukuliwa vizuri kama alivyoyasema yasingetumiwa kumtia hatiani hata na Sanhedrini. Maneno yake yangeonyesha kuwa ni tamko la ovyo la kujivuna lakini siyo kufuru. Hata baada ya kuchanganywa uongo na mashahidi wa uongo maneno yake hayakuwa na lo lote la kufikiriwa na Warumi kuwa ni kosa listahililo kuhukumiwa kifo.TVV 396.4

  Mwishowe washitaki wa Yesu walichanganyikiwa, wakawa kama wenda wazimu. Ilionekana kuwa njama yao inashindwa. Kayafa akakata tamaa kabisa. Kitu kimoja kilibaki; lazima Kristo alazimishwe ajitie hatiani mwenyewe. Kuhani mkuu alianza kutoka kitini akiwa amekunja uso kwa hamaki; “Hujibu neno?” akaamuru; Hawa wanakushuhudia nini?”TVV 397.1

  Yesu alikaa kimya “Alionewa, lakini alinyenyekea,TVV 397.2

  Wala hakufunua kinywa chake;
  Kama mwana kondoo apelekwaye machinjoni,
  Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake;
  Naam, hakufunua kinywa chake.” Isaya 53:7.
  TVV 397.3

  Mwishowe Kayafa alimwapisha Yesu akisema: “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo Mwana wa Mungu.” Kwa ombi hilo Kristo hakuweza kunyamaza. Alijua kuwa akijibu sasa atahakikisha kifo chake. Lakini ombi lilitolewa na mamlaka kuu ya taifa, na katika jina la Mungu aliye juu. Hivyo lazima adhihirishe wazi tabia yake na utume wake. Yesu alikuwa amewaambia wanafunzi wake, “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.” Mattayo 10:32. Sasa kwa mfano wake mwenyewe akarudia somo hilo. Kila jicho lilikaziwa kwa uso wa Yesu huku akajibu “Wewe umesema; ” Ilionekana kana kwamba nuru kutoka mbinguni iliangaza sura yake iliyojaa mfadhaiko, ndipo akaongeza kusema, “lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.” Kwa muda mfupi kuhani mkuu alitetemeka mbele ya jicho kali la Mwokozi. Kamwe katika maisha yake baadaye hakusahau hili tazamo kali la Mwana wa Mungu aliyekuwa matesoni.TVV 397.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents