Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Toleo la Hiari

  Yesu angeweza kuendelea kushikilia utukufu wa mbinguni. Lakini alichagua kushuka chini kutoka katika kiti chake cha enzi, ambako alitawala malimwengu yote, ili alete uzima kwa watu waliopotea.TVV 11.1

  Karibu miaka 2000 iliyopita sauti ilisikika mbinguni, ikisema, lakini mwili uliniwekea mimi .... Tazama nimekuja (katika gombo la chuo imeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu.’ Waebrania 10:5-7. Kristo alikuwa karibu kuja katika ulimwengu wetu, akiwa katika hali ya kibinadamu. Kama angekuja na utukufu wake, jinsi alivyokuwa hapo kwanza kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu huu, sisi tusingaliweza kuuvumilia utukufu huo, ila tungeliteketezwa tu. Utukufu wake ulifunikwa kabisa, na Uungu wake ukafichwa, akawa katika hali ya kibinadamu hasa.TVV 11.2

  Kusudi kubwa hili lilikuwa likionekana kwa njia ya mifano tu. Kichaka kilichowaka moto, ambapo Kristo alionekana kwa Musa, kilimwonyesha Mungu. Kichaka cha kawaida ambacho hakikuonekana na mvuto wowote, kilifunika ukuu wa Mungu. Mungu alifunua utukufu wake kwa Musa kwa njia ya kichaka kiwakacho moto, ili Musa apate kuona na kuishi, asife. Vivyo hivyo na nguzo ya wingu wakati wa mchana, na nguzo ya moto wakati wa usiku, zilifunika utukufu wa Mungu, ili wanadamu wapate kuangalia na kuishi, wasife. Hali kadhalika Kristo naye alikuja katika hali ya kibinadamu, ili watu wamwangalie, wasife. Alikuwa ni Mungu aliyekuja katika hali ya kibinadamu, ambaye utukufu wake ulifunikwa, ili awakaribie watu wenye matatizo, wenye dhiki. Katika safari ya Waisraeli ya kutangatanga jangwani mfano wa Mungu, ambao ni hema takatifu ulikuwa pamoja nao. Soma Kutoka 25:8. Hivyo Kristo aliweka hema lake kando ya mahema ya watu ili kuzoeana na sisi. “‘Naye Neno akafanyika miwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee, atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.’ Yoh. 1:14.TVV 11.3

  Tangu Yesu alipokuja na kukaa na sisi, kila mtu ambaye ni mzao wa Adamu atafahamu kuwa Mwumbaji wetu ni rafiki wa wenye dhambi. Kila aina ya mvuto wa Kimungu katika maisha ya Mwokozi alipokuwa hapa duniani, tunaona kuwa, “Mungu pamoja nasi”.TVV 11.4

  Shetani anaeleza sheria, au kanuni ya Mungu ya upendo kana kwamba ni kanuni ya ubinafsi. Asema, haiwezakani sisi kuishi. Anguko la mzazi wetu Adamu, Shetani alimlaumu Mungu kana kwamba ndiye aliyesababisha. Hivyo anawaongoza watu waone kuwa Mungu ndiye asili ya dhambi, masumbuko, na kifo. Yesu alikuja kusahihisha udanganyifu huo. Alivyoishi kama mmoja wetu aliwaonyesha jinsi ya kuishi kwa kutii amri za Mungu. Kwa hiyo alitwika hali yetu yote na kuishi maisha yetu kamili. “Alifananishwa na ndugu zake katika mambo yote.” Waebrania 2:17. Kama tungepaswa kukabili jambo lolote ambalo Yesu hakulipitia ndipo Shetani angesema kuwa uwezo wa Mungu hautoshi kutusaidia. Kwa hiyo “Yesu alijaribiwa katika mambo yote, kama sisi.’ Waebrania 4:15. Alishinda kila jambo ambalo sisi tungekutana nalo. Hakutumia uwezo mwingine ambao sisi hatuwezi kuupata. Kwa kila jaribu alilishinda kwa uwezo aliopata kutoka kwa Mungu. Hakulalamikia kanuni ya Mungu kamwe. Na maisha yake yashuhudia kuwa hata sisi tunaweza kushinda tu kama yeye, kwa uwezo ule ule; na kuiti sheria ya Mungu.TVV 12.1

  Katika hali ya ubinadamu, Kristo aligusa, ubinadamu; na katika hali ya Uungu, alishikilia kiti cha enzi, cha Mungu. Akiwa kama binadamu alituwekea kielelezo cha utii; na akiwa Mungu Mwana, alitupa uwezo wa kutii. Kwetu alisema, “Nimepewa uwezo wote mbinguni na duniani pia.’ Mat. 28:18. ‘Mungu pamoja nasi’, ndio uhakika wa kutuokoa dhambini, yaani uhakika wa uwezo wa kutii kanuni za mbinguni.TVV 12.2

  Kristo alitufunulia tabia iliyo tofauti na ile ya Shetani. “Alipoonekana na hali ya ubinadamu, alijinyenyekeza, akawa mtii hata kufa, kifo cha msalaba.” Wafilipi 2:8. Kristo alitwaa hali ya mtumwa, akatoa dhabihu, na yeye mwenyewe akiwa ndiye Kuhani, na dhabihu hiyo ni mwili wake mwenyewe. “Alichubuliwa kwa sababu ya maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake.” Isaya 53:5.TVV 12.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents