Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kwa nini ilimpasa awetofauti na wengine?

    Njia ya Yesu, haikueleweka hata kwa wazazi wake. Alionekana kama mtu aliyetengwa. Saa zake za furaha zilionekana wakati alipokuwa peke yake, akitafakari viumbe. Asubuhi na mapema, kila mara alikutwa mahali pa peke yake akiomba, na kusoma neno la Mungu. Kutoka katika hapo alikuja nyumbani kuendelea na shughuli zake za kila siku.TVV 44.3

    Mariamu aliamini kuwa mtoto mtakatifu aliyemzaa, ndiye Masihi bila shaka, walakini hakuthubutu kusema hivyo. Katika maisha yake yote alikuwa mshiriki wa mateso. Mariamu aliangalia kwa huzuni jinsi alivyokuwa akitendewa mambo ya ujeuri; katika utoto, na ujana wake wote. Kwa kuona alivyokuwa akitendewa isivyo haki, Mariamu pia alikuwa katika hali ya msukosuko daima. Alishughulika na maangalizi ya kuwalea watoto ili wawe na tabia njema. Watoto wa Yusufu walifahamu hayo, na kwa kutaka kumsaidia walitaka Yesu awe kama wao pia.TVV 44.4

    Kila mara Mariamu alimwonya Yesu, alimtaka akubaliane na mambo ya waalimu ya Kiyahudi ambao ni walimu wakuu. Lakini yeye hakukubali kugeuza tabia yake ili kupunguza matatizo yanayomkabili, maana kwa kufanya hivyo angalihafifisha kazi ya Mungu. Makuhani na walimu walipomtaka amrekebishe Yesu alikuwa katika matatizo makubwa sana. Lakini alitulia aliposoma neno la Mungu linalomwunga mkono.TVV 44.5

    Wakati mwingine Mariamu alisitasita baina ya Yesu na ndugu zake, ambao hawakuamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, lakini ushahidi ulikuwa wazi kuwa yeye ni wa Mungu. Maisha yake yalikuwa kama chachu katika jamii. Aliishi kati ya watu wafedhuli, wajeuri wasiokuwa na huruma, wakafiri, wapotevu, lakini yeye hakuchafuliwa na maovu hayo. Alichanganyika na watu wa kila hali: Askari, Wasamaria, Wapuuzi, wakulima, wenye jeuri, lakini akiwa safi. Alisema maneno ya huruma alipowaona watu katika laabu. Alijifunza upendo wa Mungu katika viumbe.TVV 44.6

    Aliwafundisha kujiangalia kuona vipawa walivyopewa. Alifundisha kuwa kila dakika ina thamani, nayo ingeonekana kuwa ni mali kuu, inayopaswa kutumiwa kwa makusudi matakatifu. Hakumwona mtu yeyote kuwa hana faida; ila alimtia nguvu kila mtu na tumaini. Akawaambia kuwa, kila mtu anaweza kupata na kutenda mambo ya faida. Kila mtu anaweza kupata tabia halisi ya kumfanya kuwa mwana wa Mungu. Kila mara alikutana na watu waliofungwa na minyororo ya Shetani, akawafariji na kuwatia tumaini.TVV 45.1

    Watu wengine Yesu aliokutana nao walikuwa katika vita na mwovu Shetani. Aliwatia moyo wasikate tamaa, maana malaika wa Mungu wako upande wao, nao watawawezesha kushinda. Wote aliowasaidia, walimtumaini, na kuona kuwa huyu ndiye msaada wetu.TVV 45.2

    Yesu alikuwa tayari kumsaidia kila mtu katika tatizo lolote alilo nalo. Kila mtu alipata utulivu rohoni mwake. Hakuna mtu aliyesema kuwa ametenda mwujiza, ila tu maneno ya amani na huruma na ya kutia nguvu na tumaini. Nguvu ya kuponya ilitoka katika kinywa chake. Hivi kwa njia hii aliwatumikia watu tangu utoto wake.TVV 45.3

    Hata hivyo, katika maisha yake, tangu utoto, ujana, na utu uzima, Yesu aliishi peke yake. Katika uaminifu, na usafi wa roho, hakuwa na mwenzake. Soma Isaya 63:3. Alijua kuwa pasipo makusudi kamili katika tabia na kanuni, ulimwengu ungepotea. Akijitoa kamili juu ya kuokoa ulimwengu, aliendesha mpango wote katika maisha yake, apate kuwa nuru ya wanadamu.TVV 45.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents