Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  59 — Makuhani na Wakuu Wanaendelea na Njama Yao

  Habari za kufufuliwa kwa Lazaro mara moja zilifikishwa Yerusalemu. Wakuu wa Yerusalemu walikuwa wakipashwa mambo yote ya matendo ya Yesu kwa njia ya wapelelzi. Baraza la Sanhedrini lilikusanyika mara moja ili kuamua mambo kuhusu jambo la Lazaro. Mwujiza mkubwa huo umefanywa na Mungu kuwa uthibitisho kuwa alimtuma Mwanawe ulimwenguni ili kuleta wokovu kwa watu. Hicho kilikuwa kielelezo cha wazi cha Mungu cha kutosha kuwaaminisha watu, na kuwaondolea mashaka.TVV 302.1

  Lakini Makuhani walikasirishwa tu na mwujiza huu. Mtu aliyekufa amefufuliwa mchana kabisa, na mbele ya mashahidi wengi. Hakuna fumbo lolote lililokuwako. Kwa sababu hii Makuhani waliazimia kumkomesha Yesu kabisa asiendelee na kazi hii.TVV 302.2

  Masadukayo hawakuwa na nia mbaya sana kwa Yesu kama Mafarisayo walivyokuwa, lakini wakati huu hao wamejiingiza pia. Hawakuamini juu ya ufufuo wa wafu, wakisema kuwa haiwezekani kumfufua mtu. Lakini kwa mafundisho ya Kristo, walijionyesha kuwa hawajui maandiko wala ufufuo wa wafu, utokanao na uwezo wa Mungu. Mtu anawezaje kufufuka kutoka kaburini? Lakini sasa mwujiza huu wa Lazaro hauwezi kubishiwa. Baada ya ufufuo wa Lazaro ndipo Masadukayo waliamua kumkomesha kwa kumwua.TVV 302.3

  Mafarisayo waliamini juu ya ufufuo, wala hawakuona kuwa kumfufua mtu kulikuwa uthibitisho wa kuwa Masihi. Lakini tangu mwanzo aliwabomolea ukuta uliowaficha kwa hiyo walimchukia. Dini safi aliyofundisha iliwafunua wakawa uchi, hivi walitaka kulipiza kisasi. Mara kadhaa walitaka kumpiga kwa mawe, lakini yeye akatoweka.TVV 302.4

  Mafarisayo walimshitaki kwa Warumi kuwa ni mtu anayetaka kuingilia mamalaka yao, na hayo waliyasema ili kufanya serikali imwangalie kwa makini. Walijaribu kwa kila njia kwamba anawashawishi watu wapate kuasi serikali. Lakini mambo yao yote yaliarrguka. Makutano walioona miujiza yake na kusikia mafundisho yake safi sana, waliona kuwa mambo ya Mafarisayo siyo ya kweli hata kidogo. Yeye si mvunjaji wa Sabato wala siyo mwenye kukufuru. Majaribio ya Mafarisayo yaliposhindwa, mwisho wakapitisha kuwa mtu akimwamini Yesu, atatengwa katika sinagogi.TVV 302.5

  Kwa hiyo Mafarisayo na Masadukayo walikuwa karibu kukubaliana katika mipango yao. Walikubaliana katika kumpinga Kristo.TVV 303.1

  Wakati huu baraza la Sanhedrini halikuwa halali kisheria. Lilikuwa baraza la usuluhishi tu. Baadhi ya wajumbe waliuliza kama wana ruhusa kumwua Kristo. Waliogopa kwamba jambo hili litaleta fujo kuu. Masadukayo walijiunga na Mafarisayo kumchukia Kristo, waliogopa Warumi wasije wakawashusha vyeo vyao.TVV 303.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents