Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  56 — Upendo wa Yesu kwa Watoto

  Yesu alikuwa mpenda watoto. Alipenda hali yao ya kitoto, kwa moyo wote. Shukrani yao ya kitoto ilimridhisha, naye alijisikia vibaya sana alipowaona wakitendewa mambo ya ufedhuli na watu manafiki. Popote alipokwenda hali yake ya wema na fadhili iliwavuta sana watoto.TVV 288.1

  Ilikuwa kawaida kuleta watoto kwa marabi ili wawabariki, kwa kuweka mikono juu yao. Lakini akina mama walipowaleta watoto kwa Yesu, wanafunzi wake waliona vibaya. Walidhani kuwa watoto hao wangali wadogo sana kuja kuongea na Yesu, kwa hiyo walidhani kuwa yeye atachukiwa. Lakini wanafunzi ndio waliochukizwa. Kwa Mwokozi aliona matatizo ya kina mama na mzigo walio nao wa kuwafundisha njia bora maishani. Yeye aliwakaribisha waje kwake.TVV 288.2

  Mara kadha wa kadha walikuja wakiwa na watoto wao wote pamoja, ili Yesu apate kuwabariki watoto wao. Yesu alisikia haja yao kwa moyo wa huruma. Lakini alingoja kwanza kuona wanafunzi watakavyowatendea. Alipoona kuwa wanafunzi waliwafukuza mama hao, aliwaonyesha kosa lao kwa kusema: “Msiwazuie watoto kunijia, hao ufalme wa mbinguni ni wao.” Aliwachukua mikononi mwake akawabariki kama ilivyokusudiwa.TVV 288.3

  Wale akina mama walifarijika kwa maneno ya Yesu wakati wa nguvu ili kubeba kazi yao kwa furaha. Akina mama wa sasa wayapokee maneno ya Yesu kwa imani kama wale mama waliofanya. Kristo ni Mwokozi wa kila mtu binafsi, na leo ni hakika yu tayari kuwapokea kama alivyofanya kwa mama wa zamani, wa Uyahudi Yesu anajua mzigo kila mama walio nao. Alisafiri mwendo mrefu ili kumridhisha mama wa Kanaani. Alimfufua mwana wa mjane, ambaye alikuwa wa pekee kwake. Na katika msalaba wa uchungu alimkumbuka mama yake. Leo masikitiko ya mama yeyote humgusa. Atafariji mwenye masikitiko yeyote na kumsaidia.TVV 288.4

  Yeye aliyesema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwakataze”, hata leo angali akiwangoja akina mama wamwendee pamoja na watoto wao ili awabariki. Hata mtoto anayekuwa angali mdogo mikononi mwa mama, anaweza kukaa kivulini mwa Mwenyezi kwa ajili ya maombi ya mama ya imani. Yohana Mbatizaji alijazwa na Roho Mtakafifu tangu kuzaliwa. Tukiunganika na Mungu, tunaweza kutazamia watoto wetu kujazwa na Roho tangu utoto wao.TVV 289.1

  Yesu aliona kuwa baadhi ya watoto walioletwa kwake siku hiyo, watakuwa wafia dini, kwa ajili yake. Watu hawa watampokea kama Mwokozi wao, zaidi kuliko watu wazima leo. Bwana wa mbinguni hujibu maombi yao na kurahisisha mafundisho yao ili yaeleweke kafika hali yao ya kitoto.TVV 289.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents