Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mungu auhurumia ulimwengu uliopotea

    Vitu vyote vya kumharibu mtu vimetumiwa na Shetani, na Mwana wa Mungu akiutazama ulimwengu kwa huruma, akaona jinsi watu wamekuwa mateka ya Shetani kwa ukatili. Wameharigika na kudanganyika, wamo katika msafara wa dhiki wakienda kifoni, wala hawana tumaini wanauendea usiku ambao haupambazuki.TVV 19.6

    Miili ya binadamu imekuwa makao ya mashetani. Ufahamu, na nguvu za kufikiri, vyote vimepotoka, kama mtu aliyepagawa. Chapa ya Shetani ilichapika katika miili ya watu. Mwokozi wa ulimwengu hushangaa kiasi gani aonapo hayo yote!TVV 20.1

    Dhambi zimekuwa sayansi, na maovu yamekuwa sehemu ya dini. Uasi na ukatili vinashindana na mbingu. Dunia zisizofanya dhambi huangalia na kuona jinsi Mungu atakavyowafutilia mbali watu wa ulimwengu. Na kama akifanya hivyo, Shetani yuko tayari kuendeleza maazimio yake hata mbinguni. Alikwisha kutamka kwamba serikali ya Mungu ina walakini. Kama ulimwengu ungaliangamizwa, Shetani angemlaumu Mungu zaidi na kuongeza maasi yake katika dunia nyingine.TVV 20.2

    Lakini badala ya kuufutilia mbali ulimwengu Mungu alimtuma Mwana wake ili kuuokoa. Njia ya kuuokoa ilitayarishwa. Utimilifu wa wakati ulipofika, nao ulifika. Mungu akaja ulimwenguni. akamwaga ulimwenguni gharika ya neema ya kuponya, ambayo haitamalizika kamwe; mpaka mpango wa wokovu utimie. Yesu alikuja ili kurudisha sura ya Muumbaji, na kuwafukuzailia mbali mashetani waliojidai kutawala, na kutuinua juu kutoka mavumbini, na kutengeneza tabia zetu zifanane na tabia yake.TVV 20.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents