Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwujiza mkuu wa Mioyo Iliyobadilika

  Yuda katika kuchagua kikao chake mezani, alijaribu kujiweka kuwa wa kwanza, na Kristo aliyetumika kama mtumwa alimhudumia yeye kwanza. Yohana aliachwa mpaka mwisho. Lakini Yohana hakulihesabu tendo hilo kama kemeo kwake. Zamu ya Petro ilipofika, alisema kwa mshangao; “Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?” Unyenyekevu wa Bwana ulimvunja moyo wake. Alijawa na aibu kuona kwamba hakuna hata mmoja katika wanafunzi aliyejitolea kutenda kazi hiyo. Kristo akasema: “Nifanyalo, wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.” Petro hakuvumilia kumwona Bwana wake, Mwana wa Mungu akitenda kazi impasayo mtumwa. Moyo wake wote uliinuka dhidi ya unyenyekevu huu Kwa sauti kuu ya mkazo akasema, “Wewe hutanitawadha miguu kamwe.”TVV 366.3

  Kristo akasema, “Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.” Kristo alikuwa amekuja kutakasa moyo kutokana na doa la dhambi. Petro alikuwa akikataa utakaso wa kiroho uliojumulisha na ule wa chini. Kwa kweli hakika alikuwa anamkataa Bwana wake. Siyo udhilifu kwa Bwana kumruhusu kutenda kazi kwa ajili ya utakaso wetu.TVV 366.4

  Petro akajisalimisha kiburi chake. Kutengana na Kristo kungekuwa mauti kwake. Akasema, “Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia.” Yesu “akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja, ila kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote.”TVV 367.1

  Maneno haya yana maana zaidi ya usafi wa mwili. Utakaso wa kiroho unaofananishwa na kuoshwa miguu. Yeye aliyekwisha kuoga yu safi lakini miguu iliyovaa kubazi mara ilihitaji kuoshwa tena. Kwa hiyo Petro na wenzake walikuwa wameoshwa katika chemchemi kuu iliyofunguliwa kwa ajili ya dhambi na uchafu. Lakini majaribu yalikuwa yamewaweka katika uovu, na hivyo walihitaji utakaso wa neema ya Kristo.TVV 367.2

  Yesu alitamani kusafisha mafarakano, wivu na kiburi kutoka katika mioyo yao. Jambo hili lilikuwa muhimu sana kuliko kuosha mavumbi kutoka katika miguu yao. Kwa roho waliyokuwa nayo, hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kushirikiana na Kristo. Wasipokuwa wanyenyekevu na wenye upendo hawatakuwa tayari kushiriki katika huduma ya ukumbusho ambayo Kristo alikuwa anaianzisha. Kiburi na kujitafutia makuu husababisha kufarakana, lakini yote hayo Yesu aliwasafisha wakati alipowatawadha miguu. Badiliko la hali lilitendeka. Yesu aliweza kusema; “Nanyi mmekuwa safi.” Sasa kulikuwa na umoja wa moyo, na kupendana. Isipokuwa Yuda, kila mmoja alikuwa tayari kumuachia mwenzake nafasi ya kwanza. Sasa wangaliweza kupokea maneno ya Kristo.TVV 367.3

  Hata sisi tumeoshwa kwa damu ya Kristo, walakini mara kwa mara moyo huchafuka. Lazima mioyo yetu michafu iletwe kwa Kristo! Mara ngapi tunamhuzunisha kwa ajili ya mioyo yetu yenye hasira mbaya, ubatili wetu, na kiburi chetu! Walakini upungufu wetu wote na uchafu wote lazima tuvilete kwake. Yeye peke yake aweza kututakasa.TVV 367.4

  Baada ya Kristo kuwatawadha wanafunzi miguu, allisema: “Je! mmeelewa na hayo niliyowatendea? Ninyi mwaniita, Mwalimu, na Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi, mtende vivyo. Amin, amin nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko Bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.”TVV 367.5

  Kristo mwenyewe alitoa kielelezo cha unyenyekevu ili watu wasipotoke na kufuata hali zao za ubinafsi. Yeye Mwenyewe akiwa yu sawa na Mungu, alitenda kama mtumwa kwa wanafunzi wake. Kristo ambaye kila goti lazima kumpigia, aliinama kutawadha miguu ya wale waliomwita Bwana. Alitawadha miguu ya msaliti wake.TVV 368.1

  Mungu haishi kwa nafsi yake. Yeye daima huwahudumia viumbe vyake. Yesu alipewa kusimama mbele ya jamii ya Wanadamu, kusudi kwa kielelezo chake apate kulundisha maana ya kuwa mhudumu. Aliwahudumia wote, na kuwatumikia wote. Kwa hiyo aliishi kwa sheria ya Mungu, na kwa kielelezo hicho alituonyesha jinsi ya kuitii.TVV 368.2

  Yesu alipomaliza kuwatawadha wanafunzi, miguu, alisema, “kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.” Kwa maneno hayo Kristo alikuwa anaanzisha utaratibu wa huduma ya kidini. Kwa tendo hilo la Bwana wetu huduma hii ya unyenyenevu ilifanywa kuwa agizo takatifu. Ilipaswa ishikwe, na kuadhimishwa na wafuasi wake ili kukumbuka fundisho hilo la unyenyekevu na huduma yake daima.TVV 368.3

  Agizo hili lilikuwa maandalio ya Kristo ya ushirika mtakatifu wa meza ya Bwana. Wakati kiburi na ufedhuli na mashindano ya vyeo, vinapopendelewa, hatuwezi kuwa tayari kushiriki meza takatifu ya Mwili na damu Yake. Kwa hiyo Yesu aliweka huduma ya unyenyekevu kuwa kitu cha kwanza, kabla ya meza ya Bwana.TVV 368.4

  Katika moyo wa mwanadamu kuna hali ya kujitukuza mwenyewe na kujiona kuwa bora kuliko mwenzake; kujipendelea, kutafuta ukuu; na mara nyingi huwa na matokeo ya dhana potovu na chuki. Huduma ya kutawadha inayotangulia meza ya Bwana inakusudiwa kumwondoa mtu katika ubinafsi, kumshusha kutoka katika kujiinua nafsi, na kumleta katika unyenyekevu utakaomwezesha kumhudumia ndugu yake. Mwonaji mtakatifu kutoka mbinguni huwapo katika huduma hii kuifanya kuwa ya kutafakari mambo ya kiroho kujutia dhambi na kuwa na uhakika wa msamaha wa dhambi. Kristo huwapo kubadilisha mkondo wa mitiririko wa mawazo ya ubinafsi.TVV 368.5

  Kadiri unyenyekevu wa Mwokozi kwa ajili yetu unavyokumbukwa, huwa mnyororo wa kumbukumbu, hutujia, kumbukumbu za wema wa Mungu na upole wa rafiki zetu wa duniani. Mibaraka iliyosahauliwa, na fadhili zilizodharauliwa hukumbukwa upya. Upungufu wa tabia, kupuzia wajibu, kutokuwa na shukurani, na ubaridi vyote huletwa katika kumbukumbu. Nia zetu huamshwa upya, ili kuvunja kila kizuizi kilichosababisha utengano. Dhambi huungamwa; na kusamehewa.TVV 368.6

  Neema ya Kristo iongoayo huivuta mioyo pamoja. Tamaa huamshwa katika kutafuta maisha ya juu ya kiroho. Moyo huinuliwa. Hivyo huweza kushiriki Meza ya Bwana, mwanga wa haki ya Kristo ukiwa umejaza hekalu la moyo.TVV 369.1

  Kwa wale wanaopata roho ya huduma hii, haiwezi tena kuwa tu tamasha. Kila huduma hii itakapofanyika kwa moyo wa kweli, watoto wa Mungu watafanya agano kwamba maisha yao yatatolewa katika huduma ya ukarimu kwa wengine.TVV 369.2

  Ulimwengu umejaa wale wanaohitaji huduma yetu. Wale walioshiriki pamoja na Kristo katika chumba cha ghorofa wataondoka kwenda kuhudumu kama Alivyofanya. “Mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda.”TVV 369.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents