Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Roho Mtakatifu Afanikisha Kazi Yao

    Kwa njia ya Roho Mtakatifu ushuhuda wa wanafunzi ulikuwa uthibitishwe kwa ishara na miujiza. Miujiza haitafanywa na mitume peke yao, bali na wale wote watakaopokea ujumbe wao. “Kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; washika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono iuu ya wagonjwa nao watapa afya.” Marko 16:17, 18.TVV 464.2

    Nyakati hizo watu wabaya hawakusita kuwaondoa kwa sumu wale waliowazuia kutimiza malengo yao. Yesu alisema kuwa wengi watadhani kuwa, kuwaua mashahidi wake ni kumfanyia kazi Mungu. Kwa hiyo aliahidi kuwalinda na hatari hii. Aliwaahidi majaliwa mapya: wanafunzi walipaswa kuhubiri kwa mataifa mengine, na hivyo watapewa kipawa cha lugha zingine Mitume na wasaidizi wao walikuwa watu wasiyo na elimu lakini kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Aliyemwagwa katika siku ya Pentekoste hotuba zao iwe ni katika lugha yao au ngeni, zilikuwa safi, sahihi, kwa maneno na :fasihi.TVV 464.3

    Hivyo Kristo aliwapa wanafunzi wake vifaa vya kufanyia kazi vilivyo kamili, naye mwenyewe alichukua jukumu la kuifanikisha. Aliwaagiza, Enendeni mkawafanye mataifa yote. Enendeni kwa kila sehemu ya ulimwengu inayokaliwa lakini mkijua kuwa kuwako kwangu kutakuwepo. Fanyeni kazi kwa imani na tumainiTVV 464.4

    Agizo la Mwokozi huwahusu waumini wote mpaka mwisho wa wakati. Ni kosa kubwa kudhani kwa kazi ya kuokoa roho inawategemea wachungaji wenyewe. Kanisa lilianzishwa kwa ajili ya kufanya kazi hii. Wote wanaochukua imani hii wanayo dhamana ya kuwa watenda kazi pamoja na Kristo. Potelea mbali mtu awe na kazi gani, jukumu lake la kwanza linapaswa kuwa, kuongoa roho kwa ajili ya Kristo. Inawezekana asiweze kuhutubia mikutano, lakini anaweza kutenda kazi kwa mtu mmoja mmoja. Mbali na karibu kuna roho zilizolemewa na hatia. Siyo maisha magumu au umaskini vinavyodalilisha wanadamu. Ball ni hatia, kutenda uovu. Kristo anatamani watenda kazi wake wahudumie roho zinazougua kwa dhambi.TVV 464.5

    Kila mtu ni lazma aanzie pale alipo. Katika jamaa zetu wanaweza kuwamo watu walio na njaa ya mkate wa uzima. Katika ujirani wetu wanaweza kuwapo walio makafiri. Kazi ikitendeka kwa imani matokeo yake yatasikika duniani pote. Mungu mara nyingi hutumia njia za kawaida ili kuleta mafanikio makubwa. Mtenda kazi aliye mnyenyekevu akiongozwa na Roho Mtakatifu atagusa kamba ambazo zitatoa wimbo utakaoenea katika vizazi vyote.TVV 465.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents