Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mawazo yaliyopotoka kuhusu Masihi na kuja kwake

    Watu wengi walioishi Yerusalemu walijisikia kuvutwa na nguvu isiyozuilika. Walijisikia kuamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Lakini Shetani alikuwa tayari kuwatilia mashaka. Iliaminika kwamba Yesu angezaliwa katika Bethlehemu, lakini baada ya muda angetoweka, na mara yake ya pili angekuja bila kujulikana atokako. Si watu wachache walioamini kuwa Masihi asingekuwa na uhusiano na binadamu.TVV 259.2

    Watu wengi walipokuwa wakitangatanga katika mashaka, Yesu alisema: “Mnanijua, na mnajua nilikotoka? Mimi sikuja kwa shauri langu, aliyenituma ni wa kweli naye hamumjui” Maneno ya Yesu yalikuwa marudio ya madai yake kwa baraza kuu la Sanhedrin, miezi mingi iliyopita, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. Kati ya watu wengi walioamini walisema: “Je Kristo ajapo hatafanya miujiza mingi kuliko hii ifanywayo na mtu huyu?” Wakuu na Mafarisayo wakiangalia hali ya mambo yalivyo waliona hali fulani mkutanoni. Waliharakisha kwenda kwa makuhani wakuu ili kufanya mipango ya kumkamata akiwa peke yake, maana waliona kuwa watu wanamwunga mkono, kwa hiyo wasingeweza kumkamata wakiwapo watu.TVV 259.3

    Watu wengi walioamini kuwa ni Masihi, walipotoshwa na hoja za uongo za makuhani na marabi. Walimu hawa walikariri kuwa unabii unaomhusu Masihi atatawala katika Sayuni na Yerusalemu, naye atatukuzwa naye atatawala toka bahari mpaka bahari, na kutoka mtoni mpaka mwisho wa nchi. Isaya 24:23; Zaburi 72:8. Jambo hili liliwafanyia ulinganisho wa utukufu ujao na hali nyenyekevu ya Yesu. Kama watu wangalisoma maandiko na kujifunza wao wenyewe wasingalipotoshwa. Isaya 61 inathibitisha kuwa Kristo atatenda mambo yale yale aliyotenda. Sura ya 53 inaeleza jinsi atakavyokataliwa na watu. Na sura 59 inadhihirisha tabia ya makuhani na marabi.TVV 259.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents