Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  43 — Kristo Avunja Ubaguzi wa Mataifa

  Baada ya mapambano yao na Mafarisayo, Yesu alitoka Kapernaumu, akavuka bahari ya Galilaya, akaenda pande za kaskazini kwenye mipaka ya Foeniki. Akiangalia upande wa kaskazini aliweza kuona miji ya zamani ya tiro na Sidoni; na mahekalu yao ya kimizimu. Ng’ambo yake kulikuwa na bahari ya mediteranean ambako wajumbe wa Injili watakwenda kuhubiri katika miji yake iliyo mikubwa ya ulimwengu. Akiona kazi iliyokuwa mbele yake, ilimlazimu kuwatayarisha wanafunzi wake watakaochukua kazi hiyo mpaka huko.TVV 222.1

  “Tazama mwanamke wa Kikanani kutoka katika sehemu hizo, alikuja akilia na kusema, Ee Bwana, mwana wa Daudi nihurumie; binti wangu anasumbuliwa na pepo mchafu.” Watu wa sehemu hii walikuwa waabudu sanamu, ambao walikuwa wakidharauliwa na kuchukiwa na Wayahudi. Mwanamke aliyekuja kwa Yesu alikuwa mmizimu, kwa hiyo alikuwa ametengwa kwa fadhili zilizowastahili Wayahudi.TVV 222.2

  Kazi ya Kristo ilikuwa imeenea mpaka katika sehemu hiyo. Mwanamke huyu alikuwa amesikia habari za nabii, ambaye huponya magonjwa ya kila namna. Akiwa na tumaini hata kwa kuponywa binti yake, Akisukumwa na upendo wa mama, alikusudia kupeleka tatizo hilo kwa Yesu . Akaamini kuwa atamsaidia. kwa muda alijaribiwa kuona shaka, kwa kuwa huyu ni Myahudi. Lakini alisikia kuwa Yesu hajali, wala hashindwi na ugonjwa wowote. Watu wote humwendea akawaponya, matajiri kwa masikini.TVV 222.3

  Yesu alijua kuwa mwanamke huyu alitamani kumwona, kwa hiyo alijitenga katika njia yake. Kwa kumhudumia tatizo lake, alimpa fundisho alilokusudia. Kwa ajili ya hili aliwaleta wanafunzi katika sehemu hii. alitaka waone ujinga uliojaa katika miji na vijiji vilivyokuwa karibu na Israeli. Watu waliopewa nuru ya kweli, hawashughuliki kuwasaidia walio gizani. Ukuta wa ubaguzi uliojengwa na Wayahudi kwa kiburi chao, hata wanafunzi wa Yesu pia walizuiwa wasiwahudumie wenye shida kwa ajili ya ukuta wa utengano. Kuta hizi za matengano, au ubaguzi lazima zivunjwe kabisa.TVV 222.4

  Kristo alipata wajumbe wake katika taifa lililodharauliwa, ambalo lilikuwa na hali dhaifu kabisa, ambayo ilionekana katika Wayahudi. Lakini mwanamke huyu hakuwa wa hali ya namna hiyo, alikuwa na imani. Wakati Yesu alipopita kana kwamba hasikii tatizo lake, yeye alimfuata akiendelea kuomba ombi lake, akiwaudhi wanafunzi kwa ombi lake, walimwambia Yesu amfukuze. Waliona kuwa Bwana wao anamfanyia uzembe, na kwamba hali ya ubaguzi baina ya Wayahudi na Wakanani ilikuwa ikimpendeza.TVV 223.1

  Lakini Mwokozi mwenye fadhili ndiye alijibu akisema: “Sikutumwa, ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” ijapokuwa jawabu hili lilionekana kana kwamba linaunga mkono hali ya ubaguzi waliokuwa nayo Wayahudi, lakini lilikuwa laumu kwa wanafunzi ambao baadaye walielewa na kukumbuka mambo aliyokuwa akiwaeleza kuwa alikuja ulimwenguni kuwaokoa wote watakaomwamini.TVV 223.2

  Mwanamke aliongeza kuomba, hali ameanguka miguuni mwake, na kusema: “Bwana nisaidie.” Yesu akionekana kana kwamba anakataa ombi lake, alimjibu akisema: “Haifai kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” Maana yake hasa ilikuwa kwamba, si vema kushughulikia wageni na kuwanyang’anya Waisraeli mibaraka waliyopewa na Mungu. Jibu hili lingalimkatisha tamaa mwombaji. Lakini mwanamke aliona kuwa hii ndiyo nafasi yake.TVV 223.3

  Katika hali iliyoonekana kana kwamba ni ya kukataa kwa Yesu, aliona fadhili kwake, ambazo hazikuweza kufichika, akasema: “Kweli, Bwana, hata mbwa hurambaramba makombo yaliyoanguka chini ya meza za bwana zao.” hata mbwa hawaachwi bila kulishwa! Hivyo hata kama kuna mibraka mingi waliyopewa Waisraeli, je, haukuwapo mibaraka unaonistahili hata mimi? Aliangalia kama mbwa angaliavyo. Je mbwa hawezi kutazamia makombo? kama anahesabiwa kama mbwa, basi aliridhika kuwa kama mbwa, naye mara moja alimkiri Yesu kuwa Mwokozi awezaye kumfanyia yote aliyomwomba.TVV 223.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents