Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uzima katika Neno

  Uzima wa Kristo, unaoufanya ulimwengu upate uzima umo katika neno lake, kwa neno lake tu, Yesu aliponya magonjwa ya kila namna na kulukuza pepo; kwa neno lake alituliza bahari, na kufutua watu. Biblia yote humdhihirisha Kristo, naye alitamani kukaza imani ya wasikilizaji wake na wafuasi wake juu ya neno lake, yaani Biblia. Wakati yeye asipokuwapo neno lake litakuwao lenye uwezo ule ule.TVV 215.4

  Jinsi maisha yetu ya kimwili yanavyosaidiwa na chakula tulacho, hali kadhalika maisha yetu ya kiroho husaidiwa na neno la Mungu. Jinsi itupasavyo kula sisi wenyewe chakul;a cha mwili, ndivyo itupasavyo kulipokea neno la Mungu. Inatupasa kujifunza neno la Mungu kwa uangalifu sana, tukimwomba Mungu atusaidie kwa roho Mtakatifu, ili tuelewe neno lake bila makosa. Inatupsa kutafakari fungu kwa fungu na kutamhua mawazo ya Mungu anayotuwazia kuhusu fungu hilo. Tulitafakari fungu hilo mpaka litukae vizuri.TVV 215.5

  Ahadi za Mungu na maonyo anayotoa, hunihusu mimi. Jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili mimi nikiamini nisipotee, bali niwe na uzima wa milele. Maneno yote yanayotumiwa katika neno la Mungu kuhusu wokovu, hunihusu mimi. Maombi na ahadi ni vyangu. “Nimesulibishwa pamoja na Kristo, walakini ni hai; wala si mimi tena, ila Kristo huishi ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, nao katika imani ya mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu” Walatia 2:20. Jinsi imani inavyorekebisha kanuni za kweli, hufanyika kuwa sehemu yetu ya maisha na nguvu, neno hutengeneza maisha na kukuza tabia za unyofu.TVV 216.1

  Mungu atajidhihirisha kwa mtu mwenye njaa ya haki na kuuchuchumilia unyofu. kwa kadiri watu wanavyojilisha kwa neno la Mungu huharibu tabia ya asilli, ambavyo ni potofu, na hutia hali ya kikristo, ambayo ni maisha ya yesu. Roho Mtakatifu huja kama mfariji. Kwa neema ya Mungu mwanafunzi wa Biblia huwa kiumbe kipya. Upendo huwa badala ya chuki, na moyo hupata uamsho wa kimungu. Hivi ndivyo kula ule mkate utokao mbinguni. Kristo alijua tabia za wale wanaojidai kuwa watu wake, na neno lake liliwapima kama ni kweli au sivyo. Alisema kuwa ni lazima waamini na kutenda kama inavyotakiwa na kugeuzwa nia zao ili kuambatana na tabia yake. Jambo hili linahusu kuacha tamaa zote na majivuno. Ni lazima kujitoa kamili kwa Kristo. Wanaotakiwa wawe wenye kujinyima, wanyenyekevu wa mioyo, wenye kutembea katika njia nyembamba iliyopitwa na mtu wa Kalwari.TVV 216.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents