Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kusudi Kuu la Roho Mtakatifu

    Yesu alitaka kuwavuvia wanafunzi wake furaha na tumaini lililokuwa moyoni mwake. Alifurahi kwa sababu karama ya Roho Mtakatifu ilikuwa ya juu kabisa kuliko karama zote ambazo angemwuomba Baba yake kwa ajili ya watu wake. Roho anayekuja ni uwezo wa kuhuisha upya maana pasipo huo, kafara ya Yesu ingekuwa bure. Uwezo wa uovu ulikuwa ukiongozeka karne hadi karne, na utiifu wa watu kwa vitendo viovu ulikuwa unashangaza Dhambi ingeweza tu kukabiliwa na kushindwa kwa uwezo wa Nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu ambayo ingekuja katika uwezo tele wa Uungu. Roho huwezesha mambo yaliyokamilishwa na Mwokozi wa ulimwengu. Moyo hutakaswa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kristo ametoa Roho wake ili kuleta ushindi dhidi ya dhambi za kurithi na maelekeo ya kutenda uovu na kupiga chapa ya tabia yake mwenyewe juu ya kanisa lake. Sura hasa ya Mungu sharti ionekane katika wanadamu. Heshima ya Mungu, heshima ya Kristo inahusika katika kukamilisha tabia ya watu wake.TVV 380.2

    Wakati “Roho wa kweli atakapokuja, atauhakikisha ulimwengu katika habari ya dhambi na haki na hukumu.” Kuhubiri Neno la Mungu hakulafaa kitu bila kuweko kwa Roho Mtakatifu. Ni pale tu Roho Mtakatifu ana poghirikiana na ukweli moyoni ndipo huleta mabadiliko na kuanzisha maisha mapya katika mtu. Roho Mtakatifu asipoiingiza kweli katika moyo wa mtu, hakuna kuanguka mwambani na kuvunjika. Hakuna kiwango cho chote cha elimu, wala manufaa hata kama ni makubwa kiasi gani yanayoweza kuwa njia ya nuru pasipo ushirikiano wa Roho wa Mungu.TVV 380.3

    Kristo ameahidi kulipa kanisa lake kipawa cha Roho Mtakatifu, na ahadi hiyo inatuhusu na sisi kama ilivyowahusu wanafunzi wa kwanza. Lakini kama ilivyo kila ahadi hutolewa kwa masharti. Wengi wanaodai kuhusika na ahadi ya Bwana huzungumzia habari za Kristo na za Roho Mtakatifu, lakini hawana kitu. Hawatoi mioyo yao iongozwe na nguvu za mbinguni. Sisi hatuwezi kumtumia Roho Mtakatifu, Roho ndiye atutumie sisi. Lakini wengi wanataka kujiongoza -wenyewe. Ni wale tu wanaomngojea Mungu kwa unyenyekevu, ndiyo hupewa Roho. Ahadi hii ya mbaraka, ikidaiwa kwa imani, itakuia na mibaraka mingine pia.TVV 381.1

    Kabla hajatoka katika chumba cha juu, Mwokozi aliwaongoza wanafunzi kuimba wimbo wa sifa. Sauti yake ilisikika, siyo kama ya maombolezo, bali yenye furaha kamili, ikiimba wimbo wa “Sifa za” Pasaka:TVV 381.2

    Haleluya Enyi mataifa yote, msifuni BWANA, Enyi watu wote, mhimidini. Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu Na uaminifu wa BWANA ni wa milele.” Zaburi 117.TVV 381.3

    Baada ya kuimba walitoka kwenda katika Mlima wa Mizeituni. Walienda polepole wakitafakari kila mtu mawazoni mwake. Walipoanza kutelemka kuelekea mlimani Yesu alisema: “Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu, kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.” (Mathayo 26:3)1. Katika chumba kile cha ghorofani Yesu alikuwa amesema kuwa mmojawapo wa wanafunzi kumi na wawili alamsaliti, na Petro atamkana. Lakini sasa maneno yake yaliwahusu wao wote.TVV 381.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents