Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Tutawatambua Wapendwa Wetu

    Sura ya Mwokozi aliyefufuka, hali yake, usemi wake vyote hivyo wanafunzi wake walivitambua. Jinsi Yesu alivyofufuka kutoka kwa hofu ndivyo wale waliolala katika Kristo watakavyofufuka. Tutawafahamu rafiki zetu, na kuwatambua kama vile wanafunzi wa Yesu walivyomtambua. Katika hali ya utukufu wa mwili, sura zao zitabaki zile zile. Tutawata-mbua wapendwa wetu.TVV 454.1

    Yesu aliwakumbusha wanafunzi wake maneno aliyowaambia kabla ya kifo chake. “Ndipo Akawafungulia akili zao wapate kuelewa na Maandiko. Akawaambia: Ndipo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu, na mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemu. Nanyi ni mashahidi wa mambo haya.” Maisha Kristo, kifo chake na ufufuo wake, unabii ulioonyesha mambo haya, na utakatifu wa sheria ya Mungu, siri ya mpango wa wokovu, na uwezo wa Yesu wa kusamehe dhambi, yote haya lazima yahubiriwe na kujulishwa kwa ulimwengu wote.TVV 454.2

    “Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.” Kumpokea Roho kwa wingi hakukutokea mpaka baada ya kupaa kwa Yesu kwenda mbinguni. Lakini Kristo aliwavuvia Roho wake kuwathibitishia kuwa pasipo Roho Mtakatifu hawataweza kukamilisha kazi yao ya kulijenga kanisa.TVV 454.3

    Kumwagiwa Roho ni kumwagiwa maisha ya Kristo. Humwezesha mwenye kumpokea awe na sifa za Kristo. Ni wale wanaokuwa na Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani yao, na ambao maisha ya Kristo yanadhihirishwa kwao ndiyo watakaolihudumia kanisa.TVV 454.4

    Kristo alisema: “Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi wamefungiwa.” Hapa Kristo hakumpa mtu ye, yote ruhusa ya kuwahukumu wengine. Hii ni haki ya Mungu tu. Lakini katika kanisa lililopangwa huweka wajibu umpasao kila mshiriki. Kwa wale wenye kuanguka katika makosa kanisa lina haki ya kuwaonya, kuwafundisha na ikiwezekana kuwarudisha tena kuwa waaminifu. Shughulikia dhambi kwa dhati. Taja dhambi kwa jina lake. Eleza jinsi Mungu asemavyo dhidi ya mwongo, mvunja sabato, mwizi, na maovu mengine yote. Kama wakidumu dhambini hukumu unayowakatia kufuatana na Neno la Mungu hupitishwa mbinguni. Kanisa lazima lionyeshe kuwa halikubaliani na matendo ya jinsi hiyo la sivyo litamdhalilisha Bwana wake. Kanisa lazima lishughulikie dhambi kama Mungu anavyoagiza na hatua hiyo huthibitishwa mbinguni.TVV 454.5

    Lakini kuna upande wa furaha. “Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa.” Jambo hili liwe la muhimu. Mchungaji amwambie mkosaji juu ya rehema za Mwokozi. Hebu na wamtie moyo mwenye dhambi atubu na kumwamini yeye awezaye kusamehe dhambi. “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki, hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” 1 Yoh. 1:9. Hebu mkono wenye kutetemeka wa atubuye uwekwe katika mkono wenye upendo wa Yesu. Toba ya jinsi hiyo huthibitishwa mbinguni.TVV 455.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents