Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    22 — Kifungo na Kifo cha Yohana

    Yohana Mbatizaji alikuwa mtu wa kwanza kutangaza habari za ufalme wa Kristo, pia alikuwa mtu wa kwanza kupata mateso. Kutoka mahali peupe huko jangwani aliletwa gerezani, katika ngome ya Herode, kama mfungwa. Herode Antipa mwenyewe alisikia mahubiri ya Yohana yakamtetemesha sana. Herode alimwogopa Yohana, akifahamu kuwa ni mtu mtakatifu, mtu wa haki. Yohana alikemea kule kuchukuliana na Herodias, mke wa ndugu yake, ambaye ni shemeji yake. Kwa muda kitambo Herode alitaka kuvunja mawazo hayo ya uasherati, lakini Herodias alimng’angania kwa nguvu, hata akamshawishi Herode amtupe Yohana gerezani.TVV 116.1

    Hali ya gereza ilikuwa mbaya sana, nayo ilimtaabisha sana Yohana. Muda ulipopita mwingi hali, ya mashaka ikamjia. Wanafunzi wake walimletea habari za kazi ya Yesu, na jinsi makundi ya watu yanavyomfuata. Lakini kwa nini mwalimu huyu, akiwa ndiye Masihi, anisaidie katika kufungwa huku? Mashaka ambayo yasiligalimjia, yakaanza, kumjia. Shetani alifurahi kwa maneno ya wanafunzi hao ambayo yamemjeruhi roho ya mjumbe wa Mungu. Mara ngapi rafiki mkuu wa mtu hugeuka kuwa adui yake?TVV 116.2

    Yohana Mbatizaji alimtazamia Yesu kukitwaa kiti cha utawala cha Daudi. Wakati ulipopita, wala Yesu hakuonyesha dalili yoyote ya kuwa mfalme wa dunia hii, Yohana aliingiwa na wasiwasi. Alikuwa ametazamia cheo kikubwa cha kibinadamu, na uwezo. Masihi angesafisha sakafu kabisa, na kukusanya ngano ghalani., na kuyachoma makapi katika moto usiozimika. Soma Isaya 40; Mathayo 3. Sawa kama Eliya, alitazamia kuja kwa Masihi kutokee kama Mungu atajibu kwa moto.TVV 116.3

    Yohana Mbatizaji alisimama bila hofu akikemea maovu mahali pote. Alithubutu hata kumkabili mfalme Herode akimkemea kwa dhambi zake. Na alingojea Simba wa Yuda aingilie kati na kumwokoa. Lakini Yesu alionekana akitulia tu, akifanya kazi ya kuponya watu na kufundisha. Alikuwa akila na watu huku mzigo wa Warumi ulizidi kuwakandamiza watu, ambavyo mfalme Herode na wenzake waliendelea kufanya wapendavyo, na kilio cha maskini na wenye dhiki kikipanda mbinguni.TVV 116.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents